Wakati Rais Donald Trump akiwa anatimza siku ya 100 toka kushika madaraka ya nchi ya marekani januari 20 2017,Utawala wa korea kaskazini leo umeamua kumkaribisha Trump kwa kutimiza siku 100 kwa kupiga bomu la majaribio la nyuklia upya licha ya makatazo makali toka mataifa mbalimbali ikiwemo marekani yenyewe.
Marekani ilishasema iko tayari kwa kuivamia korea kaskazini iwapo itaendelea na tabia hiyo ya kurusha mabomu baharini kwa kutaka kufanikisha lengo lake la kupata bomu litakaloweza kufika marekani kabisa.
Korea kaskazini wanaonekana kupuuza agizo hilo na kuonyesha ubabe kwa kupiga bomu hilo leo upya licha kuonekana halikuwa na mafanikio sana kwa kushindwa kufikia lengo hilo.
Wakati huo huo Trump amekuwa akisema maisha yake binafsi ya awali kabla ya urais yalikua bora zaidi na ya amani kuliko ndani ya urais kwani mfumo wa urais wa marekani ni mgumu sana kwa kufanya maamuzi mbalimbali, Maneno haya yametolewa na Trump baada ya kushindwa kuondoa sheria ya bima ya afya kwa wamarekani wote iliyoasisiwa na Rais Barrack Obama aliita Obama Care.
0 Comments "TRUMP ATIMIZA SIKU 100 HUKU KOREA KASKAZINI WAKIRUSHA KOMBORA LA MAJARIBIO"