
Kura za maoni zilizoonekana kulerta utata mkubwa ndani na nje ya uturuki kwa mda mrefu hatimaye waturuki wenyewe wameamua kusema ndio kwa Rais wao kuwa apewe mamlaka zaidi ktk utawala wa nchi hiyo.
Asilimia 51.4% ya waturuki wamesema ndio na 48.6 wamesema hapana na kufanya waliosema ndio kuwa wengi hivyo kufanya azima yao hiyo ya kumpa nguvu Rais kufanikiwa. usiku kucha wanachama wa chama tawala wamekesha wakisheherekea ushindi huo wakiwa rais wao Tayyip Edorgan.

Zaidi ya sheria 18 ndani ya katiba yao zitabadilishwa ili kukidhi haja hiyo ya kufanya mabadiliko hayo ya nguvu,baadhi ya mambo yanaytokusudiwa kubadilishwa ni kuondolewa kwa cheo cha waziri mkuu na kumuweka makamu wa rais tu,umri wa kupiga kura kutoka 25 ya sasa hadi 18,kuongeza idadi ya wabunge na majimbo kutoka 500 yasasa hadi 600,kuondoa nguvu ya maamuzi kutoka baraza la mawaziri na kuondoa nguvu ya bunge ktk maamuzi kwenda kwa rais.
Tayyip amezitumpia maneno makali nchi za magharibi kwa kutaka kukwamisha mafanikio ya kupiga kura hiyo kwa kuzuia waziri wake wa mambo ya nje kwenda ndani ya mataifa yao lakini hata hivyo wamefanikiwa licha ya maadui hao wa ndani na nje.
0 Comments "WANANCHI UTURUKI WAAMUA KUMPA RAIS EDORGAN NGUVU ZAIDI YA UTAWALA"