
Rais wa Uganda Bw. Yoweri Kaguta Museven ametangaza kuwastaafisha makamanda wa jeshi waliohudumia jeshi hilo kwa mda mrefu toka kuingia kwake mararakani mwaka 1986 baada ya vita ya mda mrefu ya msituni iliyofanikisha kumondoa kwa kumpindua Aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw.Milton Obote.
Yoweri alieingia madarakani kwa kupitia kikundi chake cha NRM (National resistance army) aliwachagua wanamgambo wengi waliokuwa mstari wa mbele ktk mapigano ya kuangusha tawala iliyokuwepo na kuwa makamanda wa ngazi za juu sana ktk sekta mbalimbali za utawala.

Wengi wao kwa sasa wamekuwa na umri mkubwa sana kiasi cha kuvuka umri huo wa kustaafu licha kuwa walikuwa wanaomba kustaafu wenyewe kwa mda mrefu bila mafanikio yeyote yale kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi ikiwa kufanya mazoezi na maamuzi sahihi.
Rais Museveni kwa sasa amekubaliana na maombi hayo na amezamilia kuwabadili makamanda wote wa jeshi na kuweka wapya.
0 Comments "MUSEVENI KUSTAAFISHA MAKAMANDA WA JESHI WALIOMUINGIZA MADARAKANI"