
Wataalam wa mambo ya afya duniani wanazungumzia mengi juu ya ugonjwa huu wa ukimwi ambao ulianza kugundulika miaka ya 1980 na kuanza kuasambaa kwa kasi kubwa duniani kote kutokana na tabia ya wanadamu kusafiri hukuna huko kisha kukutana kwa njia ya kujamiiana baina yao.
Njia kuu za kuambukiza ugonjwa huu ni kupitia tendo la ndoa,kujamiiana,ngono za aina yeyote iwe jinsia ya kike kwa kike,kiume kwa kiume au kike kwa kiume kama tulivyozoea. Ugonjwa huu ni hatari sana kwakua vijidudu au virusi vyake vinapoingia ndani ya mwili wa mwandamu na kutapakaa mwili mzima kwa mda mfupi kwa kuanza kushambulia seli hai nyeupe za kiumbe huyo ambazo ni muhimu sana kwa ulinzi au kinga kwa mwili wake juu ya mashambuli ya vijidudu vyote vya magonjwa,

Wataalam hawa wanaendelea kutueleza kuwa mtu mwenye maambukizi ya vurusi hivi anaweza kukaa navyo zaidi ya miaka 10 bila kujijua au kuonyesha dalili yeyote ile wala kuumwa chochote bila kujua endapo hatokuwa na utaratibu wa kupima afya yake mara kwa mara,wanaendelea kutujuza kuwa virusi vya ukimwi ni miongoni vya vijidudu vidogo sana vinavyoweza kuonekana kwa hadubini maalum,vina sifa ya kubadilika kitabia kila wakati na vinaweza kuwa hai au kufa kutokana na mazingira.

Mpaka sasa wataalam wa afya bado hawajafanikiwa kugundua dawa itakayoweza kutibu kabisa au kukinga watu wasipate ugonjwa huu licha ya juhudi zao za mchana na usiku wamefanikiwea kujua dawa zitakozoweza kumsaidia mtu ambae ameshaathirika na kumfanya japo kupunguza nguvu ya virusi hivi kufanya mashambulizi makubwa tu.mabaya zaidi wataalam wanaendelea kuteeleza kuwa ziko aina kadhaa za aina ya virusi hivi hatari ktk dunia.
Sehemu kubwa ya watu kutoka mabara ya afrika na asia ndio wanaongoza kuwa na idadi ya watu wengi wa walioathirika na ugonjwa huu na wengi wao kupoteza maisha haraka sana kutokana na kutokuwa na elimu ya kujikinga na ugonjwa huo,umasikini ulipindukia mipaka,kushindwa kutumia kinga na dawa hizo n.k.
Leo wataalam wanajaribu kutueleza kwa kifupi san ni kwa jinsi gani mtu mwenye maambukizi au virusi vya ugonjwa huu akiwa anatumia dawa za kupunguza makali ya mashambulizi lakini anaendelea kutumia vilevi kama pombe,sigara na vilevi vya aina zote.

Kwa kifupi hali hii ni kujichimbia kaburi la mapema sana kwani tukumbuke kuwa sumu zote zinachunjwa na ini na figo mwilini mwako sasa kitendo cha kutumia pombe huku unatumia dsawa za arvs jua unasababisha ini na figo kufanya kazi kwa nguvu na kwa haraka sana kwa mda mfupi,ikumbukwe dawa,pombe yeyote ni sumu ndani ya mwili wako,tabia ya kutumia vitu hivi vyenye sumu kali kwa pamoja ni kusababisha maafa makubwa kwa figo na ini na hatimae vitafeli na kuanza kueleta madhara kwa mwili mzima.
Madhara makubwa sasa yatakuja kutokea kwa mgonjwa nan kumsababishia kifo cha haraka ni pindi tu figo na ini vitakapofeli au kushindwa kufanya kazi zake hizo za msingi za kuchuja na kuondoa taka sumu zote mwilimi kwa mtu hivyo kumfanya mgonjwa kuvimba sehemu nyingi za mwili wake na kujaa maji na taka sumu ndani ya mwili wake huo. Hapo mgonjwa huyo hatoweza kuchukua duru yeyote ila kukimbilia kifo kabla ya mda ulikadiliwa.

Wataalam wanatushauri mara nyingi si vyema na ni hatari zaidi kwa mtu kutumia vilevi hata ikiwa haumwi kitu chochote lakini inakuwa hatari zaidi ikiwa atatumia huku anatumia dawa za aina yeyote ile,watu wengi wamejikuta wakipoteza uhai ghfla kwa kuchanganya vilevi na dawa za aina mbalimbali.
1 Comment "NINI KINAWEZA KUMPATA MGONJWA WA UKIMWI ANAYETUMIA VILEVI (POMBE,SIGARA) HUKU AKIENDELEA NA MATUMIZI YA ARVS"
Cancer