Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo 4/4/2017 ndani ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limepata taswira mpya leo baada ya Spika wabunge Mh.Ndugai kutoa taarifa ya uwepo wake ndani ya bunge hilo kama mgeni aliekuja na familia yake hasa kwa kusudio kumsindikaza mkewe Mama Salma Rashid Kikwete.Baada ya Mh.Ndugai kutoa utambulisho wa uwepo wake ndani ya ukumbi wa bunge wabunge walilipuka kwa ndelemo,vifijo na makofi walikuwa wakigonga meza kwa nguvu sana kwa mda mrefu huku wakiongeza maneno kama Tumekumisi Mh.kikwete tumekumisi sana.
Mh.Ndugai aliwanyamazishwa wabunge kwa mda mrefu bila mafanuikio ya haraka na kuamua kusema yeye amekaa ndani ya bunge kwa mda mrefu ila hajawahi kushuhudia mgeni kushangiliwa na kupokelewa kwa kiasi cha furaha ya aina ile ya leo.
Video ikionyesha Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa Bungeni.

0 Comments "UJIO WA DK.JAKAYA KIKWETE BUNGENI WATIKISA BUNGE LA TANZANIA"