MASHOGA WAANDAMANA UHOLANZI KUPINGA,MAUAJI,MATESO,MANYANYASO JUU YAO

Homosexual (homophibia) ni jina la kitaalam linalotumiwa kuwaita watu wanaojihusisha na ngono za jinsia moja ila neno shoga likiwa na maana ya kushiriki kwa mwanamme ktk vitendo vya ngono na mwanamme mwenziwe (Gays).

Aina na watu wanaoshiriki vitendo hivi vya kishoga na usagaji vimekuwa vikishamiri duniani kote hasa kwa mataifa ya ulaya na marekani ambako vilianza miaka mingi,na imefika mahali hata watu maarufu kama wanamuziki,wachezaji wa mpira na waigizaji wa  filamu wamekuwa wakijitangaza kuwa wao wanajihusisha na vitendo hivyo.

Kinachosumbua zaidi sio watu wote wala jamii nzima na imani za dini zinakubaliana na matendio haya na kufanya kuwa na ukinzani kwa watu na kuleta mitafaruku ktk jamii mbalimbali na kufanya watu hawa kuengwa na kukebehiwa na wanajamii sehemu nyingi.

Waholannzi wameandamana baada ya kuona mashoga wengi wakipigwa,wakitukanwa,wakinyanyaswa,wakiuawa na kutekwa nyara na watu wasiojulikana na kupelekwa kusikojulikana na hii imepelekea watu maarufu kuungana ili kupinga hatua hii sehemu mbalimbali hasa huko Chechnya kunakoongoza kwa mauaji na upotevu wa mashoga wengi.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MASHOGA WAANDAMANA UHOLANZI KUPINGA,MAUAJI,MATESO,MANYANYASO JUU YAO"

Back To Top