Inaweza kukushangaza na kukustua hii taarifa ya juu ya kondomu inawezaje kutumika kufanyiwa kazi nyingine tofauti na ile iliyokusudiwa na watu wa afya ya kutumiaka wakati wa kujamiina ili kuepusha maambukizi ya magonjwa ya zinaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mweza wake lakini pia kukinga upataji wa mimba au ujauzito usiotarajiwa au kupangwa.
Huko nchini Cuba ktk jiji la Havana mtaalamu mmoja wa anayehusika na kutengeneza pombe za wine mwenyewe nyumbani kwa miongo mingi sasa anajulikana kama Orestes Estevez mwenye umri wa miaka 65 amefanya maajabu zaidi baada kuumia mipira hiyo ya kondomu kama kifaa kimoja wapo kwa ajili ya utengenezaji wa pombe hizo.Uchukua siku 45 kutengeneza galoni moja la lita 20.
Mtaalam huyo mkongwe kwenye maswala hayo ya pombe hizo amekuwa akisifu sana matumizi ya kondomu ktk utengenezaji wa wine zake na kufanya kuwa maarufu,kupendwa,kusifiwa nan kununulika sana a wateja kutoka sehemu mbalimbali.
Kabla ya matumizi ya mipira ya kondomu alikuwa akitumia maputo ya kawaida lakini hayakuonyesha ufanisi kama ilivyo kwa kondomu,si jambo la ajabu sana kwa mtaalam huyu kutumia kondomu ktk utengenezaji wa pombe hizo kwani tumekuwa tukisikia kuwa pombe kama gongo,chimpumu n.k zimekuwa zikitengenezwa kwa kutumia malighafi chafu kabisa lakini watu wengi wanazipenda sana licha ya serikali kupiga marufuku utengenezaji nan matumizi yake.

0 Comments "MIPIRA YA KONDOMU YATUMIKA KUTENGENEZEA POMBE YA WINE(URABU)"