Upofu ni ugonjwa na unaompata mtu kwa kupoteza uwezo wa mamcho yake kuona tena,upofu uko wa kuzaliwa nao na ule wa kupata baada ya kuzaliwa unaosababishwa na na vitu mbalimbali.Upofu unaweza kuanza taratibu kabisa kadri ya umri wa mtu unavyozidi kusonga mbale na hali hiyo huzidi kabisa,ziko sababu za lishe,magonjwa na kimazingira ambazo zinaweza kumsababishia mtu kuwa kipofu.
Ugonjwa huu wa upofu hasa kwa nchi zetu za kiafrika uko zaidi ule wa (Mtoto wa jicho) yaani kiini cheusi cha ndani ya jicho kubadilika na kuweka rangi nyeupe na utando mbele yake hivyo kufanya mtu kushindwa na kuanza kupoteza uwezo wake wa kuona siku hadi siku.

Ugonjwa huu unatibika pindi mgonjwa anapouwahi na kufanyiwa upasuaji mdogo wa jicho na kutoa hali hiyo,lakini huko marekani kliniki moja ya magonjwa ya macho imegundua njia na mbinu mpya ya kisasa zaidi kutibu tatizo hilo.
Wao wamengundua njia mpya na ya kisasa zaidi kwa kutengeneza miwani ya umeme atakayovaa mgonjwa wa mamcho aina (Night blindness),miwani hii itakuwa na mfumo uliwekwa kutokea ndani njia za macho na kutafsiriwa vizuri kisha mgonjwa kuona tena kwa kutumia miwani hiyo.



0 Comments "MIWANI YA UMEME KUWAFANYA VIPOFU KUONA UPYA"