KUTANA NA MJI MKONGWE WA VENICE ULIPO BAHARINI HUKO ITALIA JAPO SI KISIWA

 Mji wa VENICE ulioko mkoa wa Venito nchini Italia ni miongoni mwa mji mkongwe duniani kiasi kuwekwa ktk urithi wa dunia UNESCO!

Mji huu unaundwa na visiwa vipavyo 118 vilivyopo bahari ya Adriatic hakuna Barabara hata moja bali mifereji ya maji zaidi ya 177 na madaraja yapatayo 400 ndio yanayounganisha mji na majumba yake makongwe kabisa (Gothic palaces,cathedral)

Mji huu una umri wa mikaa 1400 sawa na karne 14 toka kuanzishwa kwake na una ukubwa wa maili za maraba 160.1

Mji huu umekuwa kivutio kikubwa kwa watalii na viongozi mbalimbali wa dunia wametembelea,usafiri Mkuu ndani ya mji huu ni boti tu na kila watu watatu basi mmoja anamiliki usafiri huo.

Una umaarufu wa utalii kwa majumba yake yote yanayonekana kuelea au misingi yake kuanzia chini ya maji hivyo kuwapendeza na kuwashangaza watu Wengi sana.

Miji mingine inayofanana na huu ni ile ya Amsterdam nchini uholanzi (Netherlands) na ule wa Birmingham wa uingereza.



Image may contain: outdoor










Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KUTANA NA MJI MKONGWE WA VENICE ULIPO BAHARINI HUKO ITALIA JAPO SI KISIWA"

Back To Top