ZIJUE SIRI CHACHE KUTOKA KITENGO CHA NASA (National aeronautics and space admnistration)

Kitengo hiki muhimu kilicho chini ya rais wa marekani kilichoundwa julai 29 1958 ambapo kabla ya hapo kilijulikana kama NACA 1915-1958 kubadilishwa jina rasmi.

Shirika hili linaloshughulikia mambo ya utafiti wa anga kina waafanyakazi wasiopungua 17,345 Wengi wao wakiwa wanasayansi na wataalam wa mambo mbalimbali ya anga (Astronomists).Shirika hili lilianza mbio zake za kufika anga za mbali kwa kuanzia kufika ktk mwezi ambao uko umbali wa kilomita 384,400 na uchukua Siku 4-5 kufika huko kwa chombo kiendacho kasi


Dunia hadi pluto ni kilomita bilioni 7.5 na uchukua miaka 248.5 kufika huko.



Baada ya wanasayansi hao kufanikiwa kufanikiwa kufika mwezini 1969 sasa wanasayansi hao wanafanya harakati za kufika ktk sayari ya Mars ambayo iko umbali wa kilomita milioni 54.6 kutoka dunia ni ambapo ni mbali sana kiasi cha kutumia Siku 300 kuifikia sayari hiyo ya ya nne ktk mtiririko wa sayari zote,kwani hadi sasa wamefanikiwa kutumia vyombo mbalimbali kufanya uchunguzi ktk sayari hiyo na bado hawajafanikiwa kutumia watu huko.


Rocket ni aina ya chombo cha kisayansi na kisasa zaidi kilicho kama injini za mitambo mengine kikiwa kimeganywa ktk sehemu juu tatu yani Orbiter,Fuel tanks,Booster.
Kuna aina nyingi za Rocket zilizowahi kutengenezwa na NASA kama Saturn 1,1b,5,atlas v,delta 2,Falcon,Ares 1-5,pegasus,Taurus,Apollo13,Titan 2,Gemmin,Lunar na nyingine nyingi ambazo baadhi zilifanikiwa kufika walipotaka nyingine hazikufanikiwa kufanya hivyo na kulipuka au kupotea kabisa.
Rocket unaweza kufikia uzito paundi milioni 4.4 ikiwa tanki za mafuta galoni 1,359,000 za kimiminika cha oksijeni,226,000 za kimiminika cha Haidrojeni ambavyo hutumika kama mafuta ya kuikusukuma rocket nzima kwenda na kurudi anga za mbali.

Oksijeni inachukuliwa kwakuwa huko anga za mbali hakuna aina hiyo ya gesi,hivyo uchukuliwa kwa ajili ya matumizi ya mashine hiyo na kwa ajili ya matumizi ya watu walikuwepo ndani ya chombo hicho kwa mda wote watakakuwepo safarini anga za mbali hadi kurudi kwao duniani tena.

Matengezo ya chombo hiki ugharimu zaidi ya
Dola za kimarekani bilioni 35 na gharama za mataarisho ya kurusha ufikia dola milioni 500.
Injini ya rocket yenye nguvu ya 1000 HP inaweza kutumia Amoniumm perchlorate kama mafuta ambavyo huwa ktk hali ya kimiminika au yabisi,injini hii ukimbiza chombo kwa spidi ya kilomita elfu 42487 kwa saa moja.

Ukiacha rocket kutumika kwa ajili ya kufikia anga za mbali kwa ajili ya utafiti pia ubeba na kupeleka vyombo mbalimbali vya kisayansi na uchunguzi ikiwemo na satelaiti za ulinzi,mawasiliano na utafiti kama vile vya Hubble,International space station ISS.

Wataalam hawa wakati mwingine hukaa huko angani kwa miezi sita hadi tisa wakifanya matengenezo na marekebisho ya satelaiti zao.





















































Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "ZIJUE SIRI CHACHE KUTOKA KITENGO CHA NASA (National aeronautics and space admnistration)"

Back To Top