
Marekani leo usiku kucha imefululiza kupiga mabomu 59 aina ya Tomahak kuelekeza kami ya kijeshi ya anga ya syria ambayo inatumiwa pia na urusi ktk harakati za kutetea kuendelea kwa utawala wa Bashar Asad ambao juzi umeua zaidi ya watu 100 kwa kutumia silaha za kemikali za sarin na chlorine.
Waziri wa mambo ya nje wa urusi amekemea hatua hiyo ya marakani na kusema ni uchokozi wa waziwazi juu yao,hata hivyo amesema ni mabomu 23 ndio yamefika kambini hapo na kuharibu maneo machache.
Mataifa kama israel na ufaransa yamepongeza hatua hiyo ya kuipiga kambi hiyo ya syria kwakua inamiliki na kuficha silaha hizi nyingi za sumu zinazoleta vifo vingi nyakati moja.
Trump amezungumzia hali hiyio na kusema wamefanya hivyo kwakuwa walishamuonya sana Asad kwa mda mrefu lakini amekuwa mgumu kutii maagizo na kuendelea kutumia silaha hizo za sumu hivyo hakuna namna nyingine ile kuchukua hatua juu yao.
0 Comments "KITIMTIM CHA TRUMP CHAANZA KWA KUPIGA MABOMU 59 KAMBI YA JESHI LA ANGA YA SYRIA"