
Mmea huu kwa mara ya kwanza uligundulika ktk karne ya 11 huko ktk miinuko ya ethiopia barani afrika na kupewa jina la utani kama (magical fruit) mmea huu ulianza kutumika kama dawa na tiba kwa ajili ya magonjwa mbalimbali.
Kahawa imegawanywa ktk mimea ya aina mbili kuu yaani Robusta na Arabica licha ya kuwepo zaidi ya aina 12 za mimea hii,Aina ya robusta inamea zaidi maeneo ya afrika na ile ya Arabica inastawi zaidi maeneo ya mashariki ya kati,Arabica ndio kahawa bora zaidi duniani kuliko ile ya robusta.

Nchi nyingine ni kama tanzania,ethiopia,india,mexico,guetamala,honduras,indonesia,uganda n.k
Nchi ya marekani inaagiza kiasi kikubwa cha kahawa kuliko taifa lolote duniani,kwa siku moja zaidi ya vikombe bilioni mbili (2 billion) vya kichwaji hiki unyweka ulimwenguni kote.

Kahawa ia kilevi ambacho inamfanya mtu anayetumia kuwa mtumwa wa kuhitaji kutumia mara kawa mara (Addiction),aina hii hii ya kilevi inafahamika kama Caffein ambayo pia inapatikana ktk chai ya kawaida. aina hii ya kilevi inaamina pia kusababisha baadhi ya magonjwa kwa mwanadamu hivyo wataalam wanashauri kutokutumika sana kwa mda mrefu kwani inaweza kumletea madhara ya kiafya kama kuongeza mapigo ya moyo,kichefuchefu na kutapika,maumivu ya kichwa.


0 Comments "KAHAWA: JE WAJUA SIRI INAYAPOATIKANA NDANI TUNDA HILI?"