
Baada ya mainduzi hayo chini ya chama cha Afro shiraz party ASP Shekh karume alishika uongozi huo kama rais baada na kufikia April 7 1972 nyakati za jioni mji wa Stone town mjini unguja kwa kupigwa risasi na mtu asieyejulikana na kupoteza maisha papohapo. Karume alizaliwa August 4 1905 huko mwera zanzibar.
Kifo cha Abeid aman karume kilistua watanzania kwa ujumla kwa kuona mgawanyiko wa wazi baina ya wazanzibarti walikuwa wakibeza mapinduzi hayo na muungano baina Tanganyika na Zanzibar uliofanyika april 26 1964 na kufanya sehemu hizi kuwa Taifa moja.
Marehemu Abeid aman karume alikuwa rafiki wa karibu sana ktk uongozi wake baina yake na Mwalimu Julias Kambarage Nyerere ambaye naye alifariki oktoba 14 1999,kwa pamoja walifanikiwa kuunganisha mataifa yao haya kiuchumi,kiutawala na hata kichama baina ya TANU na ASP kuwa CCM februari 5 1977.
0 Comments "MIAKA 45 TOKA KUUAWA KWA KUPIGWA RISASI KWA SHEIKH ABEID AMAN KARUME"