YALIOJILI ZIARA MIKOA YA KUSINI:JPM AIPONGEZA SERIKALI YA MSUMBIJI KWA KUWARUDISHA WAHAMIAJI HARAMU

Ziara ya Rais John Pombe Magufuli imekuwa ziara ya kwanza ktk mikoa ya kusini toka kuapishwa rasmi kuwa mkuu wa nchi novemba 2015,Ziara hii imekua ya kipekee mwanzo na mwisho wake pia.

Rais alianza ziara yake ktk mji wa mkuranga,ikwiriri wa pwani,somanga aliongea na wananchi na kuwaahidi umeme wa uhakika ,kupita nangurukuru na hatimae kuja kuweka nanga  lindi mjini kwa siku mbili. Akiwa mkoani lindi alifungua miradi mbalimbali na kukuta matatizo ktk mradi wa maji wa ngapa ambao ulizinduliwa 2013 na kukuta haujakamilika hadi amefika yeye,Rais aliagiza mradi ukamilike ifikapo mwezi julai na ikiwezekana mtu aneyehusika na ujenzi huo ishikiliwe hati yake ya kusafiria hadi hapo mradi utakapo kamilika.

Rais alisisitiza zaidi watu kufanya kazi ikiwemo na kulima zaidi ili mavuno yawe mengi na bei ya chakula ishuke,kwa kukaa bila kufanya kazi vyakula vitaendelea kupanda bei na wasipokuwa makini watajikuta wanakufa kwa njaa.

Siku ya jumamosi machi 3 Rais aliingia ndani ya mkoa wa mtwara asubuhi na kupokelewa na wenyeji wake na wananchi wa mkoa huo eneo la bandari ya mtwara ili kufungua jiwe la msingi la ujenzi wa gati la tatu ili kutanua bandari hiyo yenye kina kirefu kuliko zote Tanzania,Gati hiyo itatumia zaidi ya shilingi bilioni 135 ktk ujenzi wake. itachukua wafanyakazi wa mkoa wa mtwara ili kuweka usawa ktk ajira.

Baada ya hapo Rais akiwa amefuatana na mkuu wa mkoa wa mtwara Bi.Halima dendego,waziri wa nishati na madini pro.Sospeter Muhongo,waziri wa Ardhi na maendeleo ya makazi Mh. william Lukuvi,waziri Makame mbalawa walielekea ktk jengo benki kuu kanda kusini (BOT) na kufanya ufumguzi wake na kuhutubia wananchi.

 Rais alienda kufungua Tawi na jengo mpya la benki ya NMB mtwara na baadae kwenda kufanya ufunguzi wa majengo  ya nyumba na biashara ya NHC yakiwa ni makazi na madua yaliyo jirani na ofisi za mkoana baada ya hapo kwenda kumpumzika ikulu ndogo ya mkoa mtwara hadi siku iliyofuatia.

Jumapili ya leo Mh.Magufuli aliendelea na ziara yake ktk kiwanda cha kuzalisha simenti cha dangote na kuazindua kiwanda hiko kisha kuwaagiza wahusika kwa apelekewe bomba la gesi haraka iwezekanavyo ili azalishe umeme,pia aliagiza apewe leseni a uchimbaji wa makaa ya mawe yeye mwenyewe dangote na kama atazalisha mengi basi mengine auze kwa wengine,Rais alizindua malori zaidi ya 580 ya kubeba mizigo ya kiwandani hapo.

Akiwa dangote umoja wa wafanya kazi wa dangote walisoma risala juu ya kupata tabu juu ya jaira zao kiwandani hap kutokana na wahindi kuendlea kushikilia kazi nyingi,Rais aliahidi kulishughulikia swala hilo pia.

Rais aalitembelea kituo cha kuzalisha umeme cha mtwara kilichopo jirani na bandari ya mtwara na kuahidi kupanua uzaishaji wake wa umeme,kituo hiki kina uwezo wa kuzalisha megawati 18 lakini kutokana na kuharibika kwa mashine moja sasa kinazalisha megawati 15.6 ambazo zinzhudumia mtwara mjini,lindi na masasi.

Mwisho kabisa majira ya saa saba leo mchana Mh.Magufuli alikuwa na mkutano wa hadhara ktk viwanja vya mashujaa na alihutubia mamia ya wananchi na kuanza na waziri william Lukuvi,Makame mbalawa na Sospeter muhongo kila mmoja akizungumzia mikakati ya wizara yake kwa mikoa ya kusini hasa mtwara kuwa kama makao makuu kwa mikoa ya kusini.

Mh.Magufuli alianza kwa kuelezea ujenzi wa barabara kutoka eneo la naliendele hadi masasi kupitia mtwara vijijini,tandahimba na newala yenye urefu wa kilometa 210 kuanza mapema hivi karibuni,uanuazi na marekebisho ya uwanja wa ndege ktk majengo,njia ya kurukia ndege,barabara ielekeayo uwanja wa ndege.

Rais aliongelea swala la wana CCM kupoteza jimbo lao la mtwara mjini na kutoa fursa kwa upinzani kuwa ilisababishwa na migogoro ya ndaninya chama,alisema kuwa tayari funzo limeatikana kwa wana CCM,alisisitiza kuendelea kutumbua majipu kwa wafanyakazi wazembe,wala rushwa,wahuni makazini na wabadhilifu wa mali za umma.

Mh.Rais alizungumzia matokeo mabovu ya 2016 darasa la nne,darasa la saba,kidato cha pili na cha nne,ktk matokeo ya kidato cha nne mtwara ilikuwa yamwisho kwa kuwa na shule 9 kati ya 10 za mwisho kitaifa,hii ilimsikitisha sana na kuwalaumu wazazi kwa kuahia watoto wafanye watakavyo hivyo aliamuru idara za elimu kushughulikia swala hilo lisijirudie tena na wazazi wawe wakali kwa watoto wasiendekeze ngoma na miziki tu.

Swala la korosho halikuachwa nyuma na kusema kuwa waliondoa kodi na ushuru za ajabuajabu ndio mana mauzo yalikua mazuri ka mwaka 2016 hivyo aliahidi kusmamia zaidi zao hilo na kuwabana wahuni wanaosababishga hasara kwa wakulima.

Wakimbizi na wahamiaji wa msumbiji ktk sakata la hivi karibuni Rais hakuliacha nyuma alizungumza kwa ukali na kuanza kusema anaipongeza serikali ya msumbiji kwa maamuzi yake kwani swala la kuingia bila kibali maalum ni kosa hivyo walistahiki kupata walichopata na itakuwa wamejifunza kwa hayo,Rais alisisitza serikali ya mkoa kuwa makini na watu wanaotoka msumbiji wawakague kani kuna uwezekano kuwa wengine si watanzania.Lakini pia hakuna sababu ya mkoa kupoteza pesa na kutuma magari kwa kwa wakimbizi hao waliojitakia wenyewe na pesa hizo zielekezwe ktk mambo mengine ya msingi.

Rais aliahirisha kikao ghafla manamo saa 10:35 jioni kutokana na hali ya hewa kubadilika ghafla kuonekana kuna viashiria vya kunyesha mvua licha ya asubuhi hadi mchana kuwa na jua kali sana.

Rais na viongozi wake waote ameondoka na Ndege ya ATCL  aina ya Bombadier mnamo saa 11:45 kuelekea jijini Dar es salaam.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "YALIOJILI ZIARA MIKOA YA KUSINI:JPM AIPONGEZA SERIKALI YA MSUMBIJI KWA KUWARUDISHA WAHAMIAJI HARAMU"

Back To Top