CYNTHIA ROTHROCK: MWANAMKE CHUMA CHA RELI KTK MAPIGANO DUNIANI

Jina hili la cynthia Rothrock haliwezi kuwa jina geni vichwani mwao hasa kwa wale wapenzi wa filamu za ngumi kuanzia mika ya 1980 hadi 2006. kazi kubwa za mwanadada huyu ni mwanamapigano ya aina mablimbali pia muigizaji wa filamu toka mwaka 1985 mpaka sasa.
Mwanadada huyu aliwahi kuwa na mahusiano na mwalimu wake wa michezo hii ya ngumi anaejulikana kama Ernest rothrock na kufanikiwa kupata mtoto mmoja tu anejulikana kama Skylar sophia Rothrock

Cynthia Ann Christine Rothrock alizaliwa tarehe 8/machi 1957 huko wilington jimbo la Delaware nchini Marekanim,kwasasa cynthia ana umri wa miaka (60),Mwanadada huyu anajua kucheza michezo ya kweli ya mapigano  na kumiliki mikanda meusi saba 7 kutoka ktk mafunzo ya ngumi za kweli ya mkanda mweusi wa Tang soo do,taekwondo,karate,eagle claw,wushu,northen shoulin,kung fu.

Cynthia aliwahi kushinda zaidi ya mapambano ya ngumi za kweli kwa  zaidi ya mara tano,kutokana na nguvu za ajabu za mwanadada huyu wa kipekee mwenye uwezo wa kupigana kwa mitindo mingi watu wanahisi inawezekana kuwa ana jinsia mbili ya kike na kiume na ya kiume kuwa na nguvu zaidi ndio mana anaweza kucheza michezo hii migumu  ya kijeshi duniani.

Cynthia rothrock ameshafanya filamu zaidi ya 80 na kushirikishwa ktk filamu nyingi ulimwenguni,cynthia amefanya filamu kama (yes madam or police assasins 1985, no retreate no surrender 2 1987,undefeatable 1994,tiger claws 2 1995,eye for an eye 1996,tiger claw 1999,duke hazrd reunion 1997,manhattan chase 2000,martial laws undercover 1990).

Kufikia mwaka huu 2017 cynthia rothrock amekuwa na utajiri usiopungua dola milioni arobaini na tisa (494614212) uliotokana na kazi zake hizo za sanaa ya uigizaji na michezo ya ngumi.

Mwanadada huyu kwa sasa anaishi huko calfornia ya kaskazini akiendelea na maisha yake  ya kawaida na akishiriki ugizaji hadi sasa.
Cynthia ndio mwanadada wa pekee aliyefikia kiwango cha juu kwa kuwa na mikanda meusi ya mapigano tofauti duniani.

Ni ukweli usiopingika mwanadada huyu amefanya filamu nyingi nzuri zilizouza zaidi duniani na kupendwa na watu wengi hasa ktk miaka ya 1990.








Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "CYNTHIA ROTHROCK: MWANAMKE CHUMA CHA RELI KTK MAPIGANO DUNIANI"

Back To Top