Waturuki waishio uholanzi wameandamana leo kupinga na kukemea kitendo kiovu cha kuzuiwa kwa waziri wa mambo ya nje wa uturuki aliekuwa ktk ziara baadhi ya nchi za ulaya ambazo waturuki wengi wanaishi kwa ajili ya kuelezea na kuwapa nafasi waturuki waishio huko kupia kura ya maoni ya kubadili katiba ya uturuki.
Waziri Mevlut cavusolglu alizuiwa kutoka nje uwanja wa ndege mda mchache tu baada ya kutua ktk uwanja huo wa Rotterdam na maafisa usalama kwa kuambiwa ilikuwa ni amri ya kiongozi wa juu wa nchi kuwa hatakiwi kuingia nchini.
Kitendo hiki kimemchukiza sana Rais wa uturuki Tayyip Edorgan na kusema waholanzi ni mabaki wa manazi na wana tabia za kinazi walizorithishwa na kamwe hawatooacha.
Mda mchache tu baada ya kumzuia waziri huyo wa mambo ya nje kuingia nchini na kuamua kurudi uturuki leo hii waturuki wa waishio uholanzi wameitisha maandamano makubwa na kuanza kupambana na vyombo vya usalama.
Katiba ambayo inakusudiwa kubadilishwa inaonekana na mataifa ya ulaya na marekani ni kama ina mpango wa kuongeza mda wa utawala kwa rais huyo wa uturuki.
0 Comments "WATURUKI WAANDAMANA KUPINGA WAZIRI WAO KUZUIWA KUINGIA UHOLANZI"