MSWADA WA KUPIGA MARUFUKU YA KUTUMIA VIPAZA SAUTI KTK ADHANA WAZUA UTATA ISRAEL

Kumezuka utata ktk bunge la israel baada ya hoja ya kutaka kupinga matumizi ya vipaza sauti kwa waislamu wakati wa kutoa adhana huko nchini israel kwakuwa wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia serikali yao juu ya kupata tabu sana wakati waislamu wanapokuwa wakitoa adhana mara tano kwa sikum moja.

Moja ya mbunge mwenye asili ya kiarabu mwenye kuishi ndanin ya israel alifika hatua ya kuchana karatasi iliyokuwa na mswada huo kuonyesha hasira zake kisha kutolewa nje na wanausalama wa bunge baadae kwa kitendo hiko.

Waziri mkuu  wa israel Bw. Benjamin Netanyau amesisitiza kusimamia muswada huo kwani raia wamekuwa wanashindwa kupumzika wakati wa mchana kutokana na kelele hizo za adhana ktk vipaza sauti.

Wataalam wa haki za kibinadamu wamesema waisrael wanafika mahali wanaanza  kuingilia haki za kuabudu na kidini na hivyo zinaweza kuleta migogoro na machafuko ktk jamii za kiarabu na wayahudi waishio ndani ya taifa hilo kwani waislamu wao hawajawahi kuingilia mambo ya kidini ya kiyahudi.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MSWADA WA KUPIGA MARUFUKU YA KUTUMIA VIPAZA SAUTI KTK ADHANA WAZUA UTATA ISRAEL"

Back To Top