WATU 49 WANUSURIKA KIFO AJALI YA NDEGE SUDANI KUSINI

Abiria wapatao 49 wamenusurika kifo leo baada ya ndege ya abiria iliposhindwa kutua vyema na kuanguka vibaya ktk uwanj wa ndege uliopo Mji wa Wau kaskazini magharibi wa sudani kusini.

Wahusika wa uwanja huo wametoa taarifa kuwa chanzo kikuu cha ndege hiyo kushindwa kutua uwanjani hapo vyema na kusababisha ndege hiyo iliyokuwa na abiria 49 na marubani kadhaa ni hali mbaya ya hewa iliyoleta ukungu mkali unaofanya hata waongoza ndege kushindwa kuona vizuri alama,majengo na njia ya kutua ndege.

Hata hivyo waokoaji waliwahi kufika eneo la ajali na kufanikiwa kuwatoa abiria na marubani wote salama.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "WATU 49 WANUSURIKA KIFO AJALI YA NDEGE SUDANI KUSINI"

Back To Top