WAKENYA WADHIHAKI NA KUKEJELI MADAKTARI WA TANZANIA

Lile sakata la mgomo wa madaktari wa nchini kenya limeanza kushika sura mbaya  zaidi baada ya waziri wa afya wa kenya kufika Tanzania wiki hii na kukutana na waziri mwenzie wa afya Ummi mwalimu kumpa taarifa juu ya kenya kuhitaji madktari wa ziada kutoka nchini.

Mapema waziri huyo alijibiwa kuwa Tanzania itatoa madaktari wapatao 500 kwa awamu ya kwanzana hao watakuwa ni wale madaktari wasio kwenye sekta ya umma na watakaokidhi vigezo.

Leo jioni ya machi 21 ktk runinga maarufu ya nchini kenya ya KTN NEWS inayomilikiwa na The stsndards ikiwa inaonysha kipindui cha kila siku cha "suala nyeti jukwaa la ktn" uliwekwa mjadala uliouliza "ni sawa kuajili madaktari kutoka Tanzania?''

Mgeni mwalikwa ktk kipindi hiko aliongea mengi juu yamda hiyo na mwisho alisema sio sawa kwa Kenya kuajili madaktari toka Tanzania kwa sababu zifuatazo:.

Tanzania haina madaktari wajuzi,wataalam na waliobobea kupita kenya,Viongozi na watanzania wengi wanaposhindwa kutibiwa kwao hupelekwa kenya,Huwezi kuchukua madaktari ktk nchi iliyo nyuma kwa elimu na ujuzi wa kada hiyo na hata kwa idadi ya vyuo vinavyotoa elimu hiyo,Tanzania iko nyuma sana ktk ujuzi wa kada hiyo,itakuwaje kenya kuchukua madaktari kutoka Tanzania wakati kenya wako zaidi ya madaktari 1400 ambao hawana ajira kabisa na wana ujuzi wa kutosha zaid kuliko walioko Tanzania,lakini mwisho kabisa mgeni rasmi alisema kuwa  Hafikirii kama chama cha madaktari kinaweza kuwasajili madaktari hao kutoka Tanzania kufanya kazi ndani ya kenya.

 kupata video hiyo fungua https://youtu.be/wDeaMqGB8tA?t=18

https://youtu.be/i9hYha6u7_4

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "WAKENYA WADHIHAKI NA KUKEJELI MADAKTARI WA TANZANIA"

Back To Top