
Watu hao walikuwa wakijihami kwa silaha za moto walimuua Bw.Kaweesi na wenzie papo hapo kwa kuwapiga risasi za hivyo mwilini na kutoweka ktk mazingira ya kutatanisha.
Mpaka sasa sababu ya kuuwawa kwao haijajulikana ila watu walihisiwa kuhusika na mauaji hayo wamekamatwa na kuanza kuhojiwa na jeshi la polisi.
Mauaji hayo yalimstua sana Rais wa Uganda Bw.Yoweri Kaguta Museveni na kuyalaani na kusema ni vyema sana sehemu zote zenye misongamano ya watu,makutano ya barabara zote ni muhimu kuweka kamera maalum za usalama ili kujua kutunza watendaji wa matukio kama hayo ya mauaji na uhalifu ili kusaidi polisi na vyombo vya usalama ktk kutafuta ushahidi na wahusika.

Felix Kaweesi amezikwa leo na kupata heshima zote za jeshi la polisi.
0 Comments "GENERALI WA POLISI ALIYEUAWA UGANDA AZIKWA"