KAMATI YA UCHUNGUZI WA SAKATA LA UVAMIZI WA CLOUDS MEDIA YAGONGA MWAMBA

Ile kamati iliyoundwa na waziri wa Habari,utamadun, sanaa na michezo Mh. Moses Nape Nnauye ilyounwa na Hassan Abass,Frank Balile,Johaness  Nengida,Jessy Kwayu,Mabel Mabisa iliyokusudiwa kufanya kazi na kutoa majibu ndani ya saa 24 toka kuundwa kwake.








Lakini hali hakuwa kama ilivyotarajiwa Baada ya kugonga mwamba kwa kushindwa kumuona mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul makonda kushindwa kutoa ushirikiano kwa wanakamati hao toka kuundwa kwake baada ya kutafutwa na kufauatwa zaidi ya saa 18 bila mafanikio ya kuzunguza nae ili kujua ukweli na kutoa majibu ya tukio zima la mkuu wa mkoa huyo kwenda na kundi la askari ktk ofisi za clouds media siku ya ijumaa iliyopita saa nne usiku na kushutumiwa kufanya fujo ndani ya ofisi hizo.




Hata hivyo wanakamati hao mara zote walipewa majibu kuwa mkuu huyo kwasasa ana mambo mengi sana anashughulikia hivyo inakuwa ngumu kuonana,kwa upande wa clouds media wao walishahojiwa na kutoa ushirikiano wa kutosha juu ya tukio zima.

Mh. Waziri Nape Nnauye ametoa maneno ya kuwa na subira jibu litapayika na atalitangaza.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KAMATI YA UCHUNGUZI WA SAKATA LA UVAMIZI WA CLOUDS MEDIA YAGONGA MWAMBA"

Back To Top