WAFANYAKAZI TISA TBC WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTANGAZA TAARIFA ZA UONGO

Hatua hii ya kusimashwa kazi kwa wafanyakzi hao wa shirika la umma la utangazaji la TBC la nchini imefikiwa baada ya watangazaji hao waliohusika katika kuandaa,kuipitisha na kuitangaza taarifa hiyo ya uongo.

Taarifa hiyo iliyotangazwa na kituo hiko cha runinga cha taifa ilizungumzia juu ya kupongezwa kwa Rais John Pombe Magufuli na Rais wa Marekani Donald Trump kuwa ni rais anayefanya vizuri ktk utendaji wake ktk uongozi wake wa miaka miwili ktk madaraka na kuwa ni mfano wa kuigwa na viongozi wa afrika.

Taarifa hii ilipofuatiliwa ilingundulika sio kweli kuwa Trump alizungumza hivyo

na kuwaweka matatani wafanyakazi tisa  wa kituo hiko ambao ni Gabriel zakaria,Elizabeth Mramba,Ramadhan mpenda,Chunga Ruza,Alpha wawa,Leya mushi,Judica losai,Dorithy Mmari,Prudence Constatine.

Hatua hiyo ya kuwasimamisha wafanyakazi hao imechukuliwa na mkurugenzi mkuu wa Tbc ndug Ayubu Rioba kwa kuatokana na kitendo hiko cha kutokuwa makini na habari wanazozitangaza. Hii inakwenda kinyume kabisa na moto wa runinga hiyo unaosema (TBC UKWELI NA UHAKIKA)

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "WAFANYAKAZI TISA TBC WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTANGAZA TAARIFA ZA UONGO"

Back To Top