UTURUKI YAINYOOSHA UHOLANZI KWA VIKWAZO VIGUMU

Kufuatia mgogoro bainba ya uturuki na uholanzi uanoendelea kuapamba moto baada ya waziri wa mambo ya nje wa uturuki kuzuiwa ktk uwanja wa ndege wa rotterdam kwa ajili ya kwenda kuongea na waturuki zaidi ya laki ne (400000) wanaishi uholanzi juu ya mabadiliko ya katiba.

Kuna zaidi ya waturuki milioni moja na nusu (1500000) wanaishi ujerumani ambao tayari walishaongea na waziri wao,kufuatia kuzuiwa kwa waziri huyo kulisababisha Rais wa uturuki kutamka maneno makali  kwa waholanzi na kusema kuwa "wao ni mabaki ya wanazi na mafashisti tu na anawaona kama mbwa wa kinazi tu"

Rais wa uturuki ameamua kuweka vikwazo kama kufunga ubalozi wa uholanzi uliopo uturuki,kuzuia watu wote wa kidiplomasia wanaotoka uholanzi kuja ndani ya uturuki kufanya kazi mpaka hapo uholanzin watakapoleta maneno maalum ya kuiomba msamaha uturuki kwa kosa lao.

Wakati huo huo uholanzi wamesema waturuki ndio wanaopaswa kuomba msamaha waholanzi kwa kosa la kuwatukana kuwa wao ni mbwa wa mafashisti na wanazi,lakini pia rais Erdogan ameahidi kuipeleka uhalanzi kwenye mahakama ya haki za kibinadamu kuishtaki,uholanzi nao wamejibu pigo hilo kwa kuwafukuza mabalozi na wafanyakazi wengine wa uturuki waliopo nchini kwao.

Kumekuwa na mvutano mkubwa kwa pande mbili hizo kwa kila mmoja kuona mwenziwe na makosa kwa kitendo alichokifanya. ndani ya uholanzi kumekuwa na maandamano ya waturuki kupinga  kitendo cha uholanzi,





Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UTURUKI YAINYOOSHA UHOLANZI KWA VIKWAZO VIGUMU"

Back To Top