VYAKULA KUPIGWA CHAPA YA UMILIKI KWA KUTUMIA MIONZI

Wanasayansi wa ulaya  hivi karibuni wamegundua njia mpya kabisa ya jinsi ya kuweka alama za umiliki na mda a matumizi kwa vyakula kwa kutumia teknologia ya mionzi au kitaalam ultra violet rays ambayo inatumika ktk mashine za kuangalia mifupa (exray) au ile itumikayo kuangalia ujauzito (ultra sound) na hata ile inayotumika kupikia ktk mashine za (microwaves).

Huku inaweza kuwa tofauti kidogo kwakua wanatumia miale au mionzi ijulikanayo kama (laser) anbayo pia hupatikana ktk mashime za kusomea pesa bandia au mashine za kuangalizia dvd,cd ktk nyumba zetu.

Mashine hii itatoa miale mikali sana ya rangi blue au nyekundu na kulilenga tunda au chakula husika na kuchora au kuandika nembo maalum ktk tunda hilo huku ikiongozwa na mifumo ya kikompyuta inayofanya kazi yenyewe.

Wataalam wameamua kufanya hivi ili kutofautisha vyakula na matunda na kujua mahali gai vinazalishwa na vitatumika kwa mda gani kwa mlaji.

Baadhi ya wataalam wa mambo ya afya wanaona kuwa hiyo mionzi au njia hii ya laser food tattooed) inaweza kuwa namadhara kwa mlaji wa vyakula vilivopitia aina hii ya alama kwani miale hii inasadika kuwa na mdahara ya kiafya kwa miili kama kuleta saratani,magonjwa ya ngozi,akili na viongo kwa mwanadamu.




Share :

Facebook Twitter Google+
1 Comment "VYAKULA KUPIGWA CHAPA YA UMILIKI KWA KUTUMIA MIONZI"

Jaman hzi technologia zingine sio

Back To Top