UJENZI WA RELI MPYA WAWATOA MACHOZI DAR

Maandalizi ya kusafisha njia itakapopita njia ya reli ya kiwango cha kati (starndad gauge) itakayoanzia Dar es salaam kupitia mkoani pwani na na kuishia Morogoro kwa awamua ya kwanza.

Kampuni na wakala wa usimamizi wa rasilimali za reli nchini (RAHCO) leo imeanza zoezi la  ubomoaji wa nyumba,vibanda na majengo yote yaliyojengwa ndani ya mita 15 Pande zote mbili za reli hizo kwani wamejenga kimakosa na ndani ya hifadhi ya reli hiyo.

Ubomoaji huo ulioanza Leo mapema asubuhi kuanzia katikati ya mji maeneo ya posta,kariakoo,ilala buguruni nakuendelea hadi  pugu umewaacha wananchi wakiwa ktk hali  mbaya kwa kukosa makazi ghafla wakidai wamestukizwa kwani mda waliopewa kuhama ni  mchache sana.

Wakala hao wamekuja wakiwa na magari ya kuboa na kuanza zoezi hilo  huku baadhi ya watu wakiwa hawajayoa mali zao ndani ya nyumba au majengo hayo.

Zoezi hili  limesababisha baadhi ya watu kulia  hata kuzimia kabisa kwa kile kinachodaiwa kupoteza Mali zao za pekee walizokuwa wakitegemea.

Zoezi hili  litapita maeneo mengi kwa watu wote  waliovamia eneo la  hifadhi ya reli.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UJENZI WA RELI MPYA WAWATOA MACHOZI DAR"

Back To Top