VITUKO VYA YAHYA JAMMEH:ASEMA ANAPONYA UKIMWI

Miongoni mwa vituko ambavyo havitosahaulika ktk kipindi cha utawala wa aliyekuwa Rais wa gambia Yahya jammeh,alitoa vituko vya mwaka wakati wa uongozi wake kwa kusema kuwa alikuwa na uwezo wa kuponywa waathirika na wagonjwa wa ukimwi kwa tiba na dawa zake za asili.

Yahya jammeh ambaye alikua na digrii ya somo la bailogia alikuwa na utaalam wa kutengeneza madawa ya asili nyingi ambazo alisema zilikuwa na uwezo mkubwa wa kuponya magonjwa mengi sugu n yasiy na tiba za hospitali.

Alipotangaza kuwa na uwezo wa kuponya ugonjwa huo wananchi wengi walimiminika kwenda kupata tiba zake na kuachana na mambo ya hospitali,lakini wengi ya wagonjwa hao hawakuonekana kupata ahueni licha ya kuanza tiba zake za kiasili.

Asilimia 2% ya idadi ya wananchi was Gambia wameathirika na virusi vya ukimwi,Toka kuanza kwa tiba yake hizo kulikua na ongezeko kubwa la vifo vya watu wanauumwa ugonjwa huo wa ukimwi,Yahya jammeh alifungua vituo vingi vya afya kwa ajili ya ya kuwaponya wagonjwa wa ukimwi.

Kwasasa kiongozi huyu amekimbilia nchi ya senegal kutokana na kushindwa kwa uchaguzi ulipita mwishoni mwa mwaka jana na kupelekea kulazimisha majeshi ya umoja wa afrika magharibi kumshinikiza kuachia madaraka kinguvu.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "VITUKO VYA YAHYA JAMMEH:ASEMA ANAPONYA UKIMWI"

Back To Top