Siku za hivi karibuni kumekuwa na ujumbe wa simu ya sauti ulitapakaa ktk mitandao na vyombo mbalimbali vya habari juu maongezi ya simu yaliofanyika baina ya mama yake wetu isaac sepetu na msanii wa vichekesho ajulikanae kama steven nyerere.Maongezi haya unapoyasikiliza kwa umakini utagundua kuwa zilikuwa n lawama kutoka kwa mama wema kwenda kwa msanii steve nyerere kwa kulaumu juu ya kutokufika kabisa kumuangalia wema sepetu wakati alipokamatwa kwa kashfa za kuhisiwa kujihusisha na madawa ya kulevya vita ambayo ilianzishwa upya na mkuu wa mkoa wa dar es salaam Mh.Paul Makonda.
Kimsingi simu hiyo kwa kiasi kukubwa ilikuwa ikielekeza malalamiko makubwa kwa steve nyerere na kutaka ajitetee kwanini hakufika kituo cha polisi kumtazama wema sepetu wakati wote wa matatizo yake,Steve nyerere alianza kwa kusema kuwa sababu kuu amabayo ilimfanya hivyo ni kuwa alipewa onyo na amri ya kuondoka ndani ya mkoa wa dar es salaam na hatakiwi kuonekana kwa mda,steve aliongeza kuwa yeye anafahamu kuwa wema hatumii madawa ya kulevya labda bangi kidogo ila anajua yuko kiongozi wa juu aliekuwa anamtaka kimapenzi na kumakatalia ndio akaamua kufanyia hivyo.
Steve aliongeza kuwa yeye na wema hana matatizo kabisa ila watu wanajaribu kugombanisha swahiba wake huyo mkubwa,aliwataja baadhi ya wasanii kuwa wao ndio wajinga,pia aliwataja baadhi ya viongozi wakiwemo mawaziri na viongozi wa upinzani kuwa alijitahidi kadri ya uwezo wake kuzungumza nao ili wema aachiwe ila mambo yalikuwa juu ya uwezo wake.
Simu hii ya sauti iliyoonekana kurekodiwa wakati wakiongea yawezekana na mama wema,steve au mtandao husika na kurushwa ktk mitandao ya kijamii na kusikika na ulimwengu mzima,kimsingi mawasiliano ya kitika simu baina ya watu wawili ni siri na haitakiwi kutolewa isipokuwa pale inapohitajika au kwa sababu maalum.
Kwa kawaida mawasiliano yote tunayoyafanya ikiwa ni mesegi au aina yeyote ile ya mawasiliano uwa yanahifadhiwa ktk mitandao tunayotumia hivyoni kosa kwa mtu kuvujisha mawasiliano hayo pasipo na sababu za msingi kwani kuvuja kwa mawasiliano hovyohovyo kwa njia mbalimbali yanaeza kuleta madhara makubwa ktk jamii ikiwemo migogoro ya ndoa na mahusiano,kuharibu undugu,ujamaa,kuumizana na wizi na hata vifo vinavyotokana na visasi,

Madhara ya kuvuja au kuvujisha kwa makusudi mawasiliano ni makubwa na mengi sana,kitendo cha maneno ya wazi na kutaja majina ya watu wengi wakubwa kwa wadogo inaweza kuleta kashfa kwa viongozi hao,lakini kikubwa ni juu ya hatari ambayo itamuandama steve nyerere ktk mwendelezo wa maisha yake kwani alichokiongea kila mtu alikisika wazi.
Napata tabu sana napojaribu kufikiria na kuwaza aliye rekodi na aliyetuma simu hii ya sauti ktk mitandao alikuwa na lengo lipi kuhusu maongezi haya,je alikuwa hajui madhara ya kufanya hivi kwa wahusika?
Watanzania tuzinduke sana na matumizi mabovu ya mawasiliano ,waligundua na kuleta wao walikuwa na lengo zuri sana la kuwaweka watu karibu ktk maendendelea na si kwa kutengeneza migogoro na vifo ktk jamii.
Kiukweli hali ya matumizi ya mawasiliano kwa sasa hasa nchi za kiafrika imefikia pabaya kwani watu wamekuwa wakifanya mambo kana kamba hawana ubongo kichwani na hawazi lolote juu ya maisha yake,ni vizuri kutafakari kwa kina kabla ya tuyma ujumbe wa sauti,picha ua video au maneno kwa jamii kwani baadhi ya jumbe zinaweza kuwa chachu ya kupelekea watu kutoelewana,kuachana na hata kuuwana.
Tangu kuingia kwa matumizi ya simu katikati ya miaka ya 1990 kumekuwa na ongezeko kubwa la mambo ya uhalifu wa mitandao,kuvunjika kwa ndoa,kujidhalilisha na kudhalilishwa mitandaoni watu wakiwa watupu,hali hii inatisha sana kiasi kwamba sasa watu wamekuwa waoga na simu kabisa kwa kuogopa kurekodiwa na kurushwa ktk mitandao bila kutaka.
Tusikulupuke na matumizi mabovu yta simu,baadhi ya programu ziliwekwa kwa matumizi maalumu ya usalama na upelelezi pindi inapobidi ila sio kila mtu anaweza kufanya hivyo kwani sheria inaweza ikakuweka pabaya bila matarajio.



0 Comments "ALICHOTENDA MAMA WEMA SEPETU KWA STEVE NYERERE NI HATARI TUPU"