MAGUFULI KUFANYA ZIARA MIKOA YA LINDI NA MTWARA KWA MARA YA KWANZA

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Joseph Magufuli leo Alhamisi tarehe 2/3 /2017 anatarajia kuanza ziara yake rasmi ktk mikoa ya lindi na mtwara ikiwa ni ziara ya kwanza toka kuingia madarakani novemba 2015 alipoapishwa kuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Ziara hii italenga zaidi ktk kukagua na kufungua miradi ya maendeleo mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ikiwemo na kusikiliz kero za wananchi wa maeneo haya.

Kikubwa mikoa  ya kusini imeballikiwa kuwa na rasilimali kubwa ya gesi na mafuta kule songosongo,mnazibay na msimbati ambayo ni muhimu kwa kuzalisha nishati ya umeme ktk nchi hii kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwanda.

Rais Magufuli ataandamana na viongozi wengine wa serikali na kupokelewa na mkuu wa mkoa wa lindi Bw, Godfrey Zambi,miongoni mwa mambo muhimu atakayofanya mkoani lindi ni pamoja na kuzindua mradin wa umeme wa kilovoti 32 kutoka ktk gridi ya taifa,kwani kumekuwa na tatizo kubwa la umeme kwa mikoa ya lindi na mtwara kwa kukatika mara kwa mara bila taarifa wala sababu rasmi licha ya kuwepo kwa matumizi ya gesi ktk kuzalisha umeme huo.

Tarehe 4 Rais anatarajia kuwepo mkoani mtwara na kupokelewa na mwenyeji wake mkuu wa mkoa mtwara Bi. Halima Dendego na kukagua miradi kama jengo la benki kuu kanda ya kusini.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MAGUFULI KUFANYA ZIARA MIKOA YA LINDI NA MTWARA KWA MARA YA KWANZA"

Back To Top