UKUMBI WA CCM DODOMA WAPEWA JINA LA (KIKWETE HALL)

Ule ukumbi mpya wa mikutano ya ccm mkoani Dodoma ambapo ndio Mji Mkuu wa nchi,makao makuu ya chama na ofisi za cha mapinduzi zilipo umepewa jina jipya Leo.

Jina hilo jipya lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John pombe Magufuli alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo ndipo Rais jpm alipomuomba Ndugu Abddulrahaman Kinana kupitisha jina la KIKWETE HALL na kuuliza wanachama wote kama wameridhia au la ! Jina hilo  lilikubalika rasmi baada ya wanachama wote  kuridhia ombi hilo.

Hata hivyo alipohutubia alisisitiza kuwa Kinana ni mtu muhimu sana ktk ujenzi wa chama hasa kwa mwaka 2015 kabla na baada ya Uchaguzi ambao ulionekana kuwa mgumu kwa chama hiko,hivyo Naye anastahiki kupewa heshima ya kipekee.

Ukumbi huo ambao ulijengwa kwa gharama kubwa ililazimu kufanya hivyo kwani kabla ya hapo mikutano ya chama hiko ilikuwa ilifanyika la chakula la
taifa la  mkoa na walikuwa wakilazimika kuhamisha magunia ya mahindi kwanza na baadae kuanza kupangilia mazingira kabla ya mkutano huo na kufanya gharama za maandalizi hayo kufikia milioni mia saba 700 ukiondoa gharama za wajumbe kama malazi,vyakula,posho na usafiri.

Kutokana na halo hiyo serikali ya awamu ya nne  iliona kuna ulazima wa kujenga ukumbi maalum ili kuepuka usumbufu na kupunguza gharama hizo.









Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UKUMBI WA CCM DODOMA WAPEWA JINA LA (KIKWETE HALL)"

Back To Top