UHURU KENYATTA:NITAAJIRI MADAKTARI KUTOKA NCHI JIRANI IKIWA MGOMO UTAENDELEA

Rais wa Kenya Uhuru kenyatta hivi karibuni ametangaza kwa umma kuwa  endapo mgomo wa madaktari uliopo utandelea kufanyika basi serikali yake itachukua maamuzi magumu juu yao kwa kuwafukuza kazi na kuajili upya madaktari kutoka Tanzania,uganda,ethiopia na hata cuba.

Madaktari wa kenya wamekuwa na mgomo zaidi ya miezi mitatu mfululizo ktk kudai kulipwa mshahara wa milioni sita na nusu kwa mwezi tofauti na ule wa sasa wa shilingi milioni nne  ambazo wamesema hazikidhi mahitaji yao na wala haifanani na kazi wanazofanya .

Madaktari hao wameendelea kusema kuwa wanasiasa wanapata mishahara mikubwa,nyumba na malupulupu makubwa zaidi kuliko wao wanaofanya kazi za msingi za kuokoa uhai wa watu siku zote na kuhatarisha maisha na afya zao.

Tangazo hili alilolioa ktk mkutano wa hadhara limekosolewa vikali na makundi mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kile kinachoonekana na kudharau au kuhatarisha maisha ya madaktari wapya wa kigeni kutoka nje ya nchi hiyo.

Umoja wa madaktari Tanzania UMAT kwa pamoja wamekataa ombi hilo la kenya kwani kukubali kwao itakuwa ni sawa na kuwakandamiza wenzao wa kenya kwakuwa hata wao wako ktk matatizo kama hayo kwa miaka mingi sana,na wameshafanya migomo mingi kuishinikza serikali kutatua kero zao ila imegonga mwamba.

Kenya imetoa siku tatu tu kwa madaktari wote kurejea kazini na baadae watazunguma habari za pesa kwani mgomo huo wa zaidi ya siku 97 sasa unaathiri sekta ya afya.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UHURU KENYATTA:NITAAJIRI MADAKTARI KUTOKA NCHI JIRANI IKIWA MGOMO UTAENDELEA"

Back To Top