MUHAMAD BUHARI AREJEA NIGERIA BAADA YA MATIBABU

Rais wa Nigeria Mh. Muhammad Buhari amerejea hivi karibuni kutoka uingereza alikokuwa ktk matibabu zaidi ya miezi miwili mfululizo na kuiacha nchi chini ya makamu wake wa rais ndugu Yemi osinbajo kwa mda wote huo.
Kiongozi huyu wa taifa hili la nigeria amekuwa akitoka ndani ya nchi yake mara kwa mara kwenda mataifa mengine kwa ajili ya matibabu ya matatizo aliyonayo ambayo yamebaki kuwa siri ya uongozi wa juu.

Mh.Muhammad Buhari mwenye umri wa miaka 74 kwasasa alyeingia madarakani 2015 baada ya kumshinda mpinzani wake ndugu Goodluck Jonathan aliyekuwa rais wa taifa hilo pia kwa kumshinda umaru mussa Yaraduwa.

Muhammad buhari amewasili jana ijumaa asubuhi na kutua ktk kiwanja cha ndege cha kijeshi cha Kaduna na kupakiwa ktk helikopa ya kijeshi hadi Abuja makao makuu ya nchi,sababu ya kushuka ktk kiwanja cha ndege cha kaduna ni kufanyiwa kwa ukarabati kiwanja cha Abuja.

Hata hivyo Rais huyo bado aliendelea kumpa madaraka makamu wa rais kushikilia madaraka hadi jumatatu ijayo atakapochukuamadaraka upya. Bado hali ya rais huyo anaonekana kudhoofu na kuwa si mwenye nguvu.

Baadhi ya makundi wamefikia mahali na kusema kwakuwa hali ya Rais inaonekana kuteteleka mara nyingi toka kuingia kwake madarakani basi ni bora akajiuzulu tu mwenyewe.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MUHAMAD BUHARI AREJEA NIGERIA BAADA YA MATIBABU"

Back To Top