SYRIA NA IRAQ ZATUHUMIWA KUTUMIA SUMU VITANI

Vita inayoendelea kupiga iraq toka 2003 na huko syria 2011 baina ya serikali za nchi hiyo na wapinzani zilizosababisha vifo vya maelfu ya watu ktk nchi hizi.
Hali ya uchumi na maisha ya watu binafsi yamekuwamagumu kwa kushindwa kutulia na kukaa kufanya shughuli za kawaida kwa kuhofia usalama wao,kumekuwa na makundi makubwa  ya raia wa mataifa haya wakikimbia nchi zao kwenda  ulaya na mataifa ya jirani.

Kikubwa kinachofanywa na majeshi ya serikali na yale ya waasi kutumia silaha za sumu hasa gasi za sarin na klorini  ambazo zinapotumika umfanya mtu kushindwa kupumua,inaunguza ngozi na kuweza kupoteza uhai wa mwasirika kwa mda mfupi sana.

Matumizi ya silaha za sumu ktk vita yalishapigwa marufuku na sheria za kimataifa miaka mingi na umoja wa mataifa UN na NATO  kwani silaha hizi ni hatari na zinaleta madhara makubwa kwa wananchi hata wasiohusika na vita hiyo.

Kumeripotiwa vifo vingi vya watu wanaokufa kutokana na athari za matumizi ya gesi hizi za sumu maeneo ya allepo,mosul,homs iliyopo syria na iraq.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "SYRIA NA IRAQ ZATUHUMIWA KUTUMIA SUMU VITANI"

Back To Top