
Rais magufuli alianza na kutembelea eneo la bandari ya mtwara kwaajili ya kuweka jiwe la msingi kufungua ujenzi wa gati mpya ya tatu inayotarajiwa kujengwa bandarini hapo,alihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria eneo hilo na kuendelea kusema kuwa serikali ina mpango na imeshasaini ujenzi wa na barabara ya kutoka mtwara mjini,vijijini,tandahimba,newala hadi masasi yenye urefu wa zaidi ya kilomita 210 utakao anza hivi karibuni.
Aidha Rais Magufuli leo hii atakwenda kufungua jengo mpya la Bank la Nmb maeneo ya mkoani,majengo la shirika ya nyumba ya taifa yalipo nyuma ya ofisi ya mkoa na yale yalio kando kando ya bahari (shangani),pia anatarajiwa kutembelea jengo la benki kuu ya kanda ya kusini.
Rais Magufuli leo atalala mkoani mtwara ikulu ndogo ya mkoa anatarjiwa kuongea na mamia ya wananchi watakahudhuria ktk viwanja vya mashujaa.
0 Comments "JPM: AANZA KUTEMA CHECHE MTWARA"