
Madaktari bingwa wanawake wa Tanzania hivi karibuni waliikaribisha siku hii adhimu ya wanawake duniani kwa kuupanda milima kilimanjaro kama ishara ya kupinga vifon vya kina mama wajawazito nchini ambavyo vinaendelea siku hadi siku licha nchi na mataifa kuweka mikakati ya a vifo hivi vinavyosababishwa na ukosefu wa huduma bora,elimu,umasikini,kuchelewa kufika vituo vya afya n.k.
Kuna taasisi kam TGNP(mtandao wa jinsia) iliyopo mabibo mwisho,TAMWA(chama cha waandishi wa habari Tanzania chin ya Edda Sanga) na TAWLA) (chama cha wanasheria wanawake Tanzania) mashirika haya ya ndani na mengine yaliopo kimataifa yapo kwa ajili ya kutetea haki za wanawake ndani na nje ya nchi kwa kuhakikisha kuwa wanawake wanapata haki zao za msingi ktk maeneo ya kazi,siasa,elimu,ktk mahusiano kwani wao mara nyingi uonekana kuwa wananyanyaswa na kuabaguliwa ktk mazingira hayo.
Kumekuwa shida ktk eneo la ndoa na mahusiano kwa kutokea kudhulumiana kwa mali,kupigwa,utoaji wa talaka na mambo ya urithi inaonekan wanawake wengi wanaathirika ktk jamii ktk nyanja hizi.
Ktk elimu na siasa au vyeo watu wengi wamekuwa na mtazamo hasi kwa jinsia ya kike kuwa wao hawawezi kufanya mambo haya kwa usahihi wake kutokana na jinsia zao,ehemu za kumekuwa na rushwa za ngono pindi mwanamke anapohitaji kazi mahala fulani na kukutana na wahusika wa kiume ndio watoa ajira hizo.
Ktk majukumu ya kazi za nyumabani pia kumekuwa na taratibu ya kubagua kazi za kiume ana za kike hivyo kumfanya mwanamke kuwa na majukumu au kazi nyingi zaidi ktk jamii kuliko wanaume.
Mila na desturi potofu kama ktk umiliki na urithi wa mali,tohara kwa wanawake(ukeketaji) na kutengwa kwa wanawake kwenye baadhi ya mambo kutokana na mila a desturi hizo pia ni miongoni awake imekuwa ni changamoto zinzzowakumba wanawake.
Afya ya uzazi kwa wanawake ikiwemo mimba za mapema au utotoni,malazi,vituo vichache vya huduma hizo,huduma mbovu,kukosekana kwa vifaa vya kujifungulia,ukosefu wa wahudumu wa afya,umbali mrefu kutoka vituo vya afya a wazazi vitokanavyo na kujifungua,elimu ndogo juu ya uzazi kwa wajawazito,ukosefu au upungufu wa wataalam wa uzazi zote ni changamoto kwa wanawake hadi leo hii ktk nchi nyingi za kiafrika na usababisha vifo zaidi ya elfu kumi na moja kwa mwaka kwatanzania (11000).
Misaada ya kisheria na elimu kwa wanawake,kumekuwa na matukio ya kunyanyswa,ubakaji,ulawiti unaofanywa na watu na kuwaweka wanawake ktk hali ngumu pindi wanapotaka misaada ya kisheria juu ya ukatili huu wa kijinsia,wengi wao wanajikuta wakipoteza ushahidi au kuogopa kuripoti ktk vituo vya kisheria kama polisi,mahakamani kwa kupata msaada kwa kuogopa jamii au kuhofia wahusika waliowatendea mamboi hayo hivyo wengi wamejikuta wakibaki na maumvu ya kisaikologia mda wote wa maisha yao.
Kifupi wanawake wana changamoto nyingi ktk maisha yao ya kikla siku ambazo serikali na jamii kwa ujumla zinapaswa kuzisimamia kwa nguvu zao zote ili kuhakikisha wanakomesha au kuamaliza kabisa changamoto hizi ktk jamii hii yta wanawake ambao ndio nguzo na wengi kwa idadi ulimwenguni kote.
0 Comments "SIKU YA WANAWAKE DUNIANI:YAAZIMISHWA KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO"