MKUU WA WILAYA AMCHAPA MAKOFI MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA

Mkuu wa wilaya ya njombe mkoani  Njombe Bi.Ruth Msafiri amejikuta akimpiga makofi mwenyekiti wa serikali  ya mtaa wa Buguruni Bw,Mtalawale Emmanuel Ngalime baada ya kutokea kwa sintofahamu kwa viongozi hao wawili.

Tukio hili limetokea baada ya mkuu wa wilaya huyo kufika ofisini hapo na kumtaka kiongozi huyo kuondoka eneo hilo na kuacha nafasi hiyo wazi kama alivyoagiza siku nyingi na kutotekeleza agizo hilo.

Mkuu wa wilaya huyu alitoa amri kwa mwenyekiti huyo mda mrefu kwa kosa lam mwenyekiti huyo kuwa na kosa la  kujaribu kubaka na kuhukumiwa kifungo cha nje kwa mda wa mwaka mmoja. Ktk sheria inamtka kiongozi yeyote wa umma kuachia madaraka pindi tu atakapkutwa na hatia na kushatakiwa na mahakama.

Agizo hilo la mkuu wa wilaya lilipingwa na mwenyekiti huyo na kumataka mkuu wa wilaya kuwaambia wananchi ndio wamtoe na sio yeye mwenye uwezo wa kumtoa na sio yeye kwakuwa hajamchagua bali alichaguliwa na wananchi, kauli hii ilimfanya mkuu wa wilaya kushindwa kujizuia na kujikuta akimpiga makofi mwenyekiti  huyo na kuagiza akamatwe na kuwekwa ndani kwa saa arobaini na nane.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MKUU WA WILAYA AMCHAPA MAKOFI MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA"

Back To Top