Kiasi cha mwezi mmoja tu uliopita Korea kaskazini iliweka ktk hali ya taharuki mataifa ya jirani yake ya korea kusini na japan kwa kurusha kombola la masafa marefu kuelekea japan na kutembea zaidi ya kilometa 550 ikiwa ni karibu ya kufika mji wa Tokyo uliopo japan. Hali hii ilisababisha umoja wa mataifa,ulaya,china na mareakani kuiwekea vikwazo korea kaskazini kwa kuendelea na tabia hiyo ya kuitibua amani ya mataifa ya asia mashariki ya bahari ya pasifiki.Jana tu korea kaskazini limerusha makombola mengine manne ya masafa marefu kuelekeza japani yenye uwezo wa kusafiri zaidi ya kilometa 1000 ikiwa kilometa mia sita tu kufika mji wa Tokyo,kitendo hiki kimesababishwa na hali ya wiki iliyopita ya Japani,korea kusini na marekani kufanya mazoezi ya pamoja ktk mipaka ya bahari ya korea kusini ikiwa ni ahadi ya raisi wa marekani kuahidi ulinzin wa kutosha kwa mataifa hayo juu ya vitisho vya silaha za kinyuklia kwa majirani zake.
Marekani meamua kuleta mtambo wake wa kurusha makombola ya masafa marefu ktk nchi ya korea kusini unaojulikana kama THAAD (Terminal high altitude area deployed) wenye uwezo wa kursha makombola kwa umabli wa zaidi ya kilometa 2000 ikiwa kama majibu kwa korea kaskazini ikiwa ataendelea na vitisho vyake.
China ambayo ndio rafiki wa karibu wa korea kaskazini amekemea uamuzi huo wa marekani kupeleka mitambo hiyo na kusema marekani na mshirika wake watakuwa na ya kujibu juu ya maamuzi yao hayo.


0 Comments "MAREKANI,KOREA KUSINI,JAPAN ZAFYATA MIKIA KWA KOREA KASKAZINI"