HOSPITALI YA KIJESHI YAVAMIWA AFGHANISTAN

Watu 30 wameuawa na zaidi ya sitini wameumia vibaya baada ya wavamizi wanao hisiwa kuwa ni Taliban au sola ya kiislam IS kuivamia hospitali ya kijeshi iliyopo mji mkuu wa nchi hiyo wa Kabul.
Shambulia hilo linaloonekana kupangiliwa kwa umakini wa hali ya juu kwa wavamizi hao kuja wakiwa wamevaa nguo za kidaktari za hospitali hiyo huku wakiwa wana mabomu na bunduki za AK 47 na kuwaweka madaktari wote chini ya ulinzi na kuua baadhi yao wakiwemo wagonjwa.

Hospitali hii ya kijeshi iliyopo jiranin kabisa na ubalozi wa marekani ilisikika milipuko mizito ya mabomu na risasi zikilindima ndani ya jengo hilo ktk mji wa Sardar daud khan,shambulio ili la kustukiza limeonekana kuwa limepangwa kwa mda mrefu  na inashangaza kwanini serikali imekuwa dhaifu kiasi hiki cha kusababisha mauaji ya watu wengi wasio na hatia.

Mpaka sasa wavamiaji hao bado wanamiliki jengo na watu wote walioko ndani  hawajatoka.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "HOSPITALI YA KIJESHI YAVAMIWA AFGHANISTAN "

Back To Top