SCOTLAND YASAKA UHURU TOKA KWA WAINGEREZA

Kwa mara nyingine tena nchi ya scotland ambayo iko ktk muungano wa uingereza (UNITED KINGDOM) yaani england,scotland,ireland  inaomba tena kufanya kura ya maonin kwa watu wake kwa mwaka 2018 na 2019 juu ya kujitenga na muungano huo

Licha ya taifa la scotland kufanya aina hiyo ya kupiga kura za maoni (REFERENDUM VOTES) kwa raia wake kwa kuuliza je wanahitaji kubaki ndani ya muungano huo au la? Watu wengi walionyesha hamasa yao ya kubaki ktk muunganon huo ambao ndio muunagano uliodumu zaidi duniani wenye miaka zaidi ya 300 toka kuungana kwake.

Nchi ya scotland imekuwa ikilalamika mara kwa mara kwa kuona kubanwa na kuzidiwa nguvu ktk maamuzi mengi ya pamoja na kufanya wao wakati mwengine kujikuta wakiingia au kutoka ktk mambo wasiyoyapenda au kupenda kwa kuzidiwa nguvu ya kura za maoni.

Mwishoni mwa mwaka 2016 uingereza ilipiga kura ya maoni kwa raia zake juu ya kujitoa umoja wa ulayan EU kwa kuona kuwa wao wanajikuta wakiumia kubeba mzigo mkubwa ktk umoja huo na kupata maslahi machache sana,jambo hili la kijitoa umoja wa ulaya liliwaweka scotland ktk wakati mgumu na kujikuta na wao wako nje ya umoja huo baada  ya waingereza wengi kupiga kura ya ndio.

Nchi hizi zenye kupakana kwa kilometa 154 tu kutoka kila upande zina historia ndefu kwa falme zilizopita kupigana mara kwa mara na hatimae kuungana.

Waziri wa kwanza wa scotland Nicola Sturgion aliufikisha ujumbe huo wa kupiga upya kura kwa mara nyingine kwa waziri mkuu wa uingereza Thereza may.

Kura hiyo ya kujitoa umoja ulaya BREXIT  ya mwaka 2016 ndio iliyochochea zaidi hali hii kwakuwa wananchi wengi wa Ireland na scotland walipiga kura ya kukataa kujitoa na umoja huo wao walihitaji kuendelea kuwepo.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "SCOTLAND YASAKA UHURU TOKA KWA WAINGEREZA"

Back To Top