SAIDA KAROLI AZUNGUZA UKWELI KUHUSU MAISHA YAKE

Mwanamuziki mkongwe anayefahamika kwa jina la  Saida karoli amejikuta akizunguza maisha yake  halisi ktk moja ya kituo cha runinga nchini.

Stori ya mwanadada huyu iliyoonyesha kutia simanzi sana kwa shida na matatizo aliyopitia ktk kipindi cha utoto wake hadi alipofikia.

Said a karoli anayefahamika kwa kuimba nyimbo zenye ala ya kihaya kama Salome,kaisiki ambazo ni maarufu pia kwa kucheza na kuvaa mavazi ya kabila la  kihaya.

Saida karoli mwenye historia kuuliwa wazazi na Ndugu zake wengi mkoani kagera kwa uvamizi aliishi kwa shida kubwa sana na kusababisha kutokwenda while kabisa na kusababisha kutojua kusoma wala kuandika mpaka anakuwa mwanamuziki.

Saida  amebahatika kupata watoto watano kila mmoja akiwa na baba yake, na mtoto wa kwanza alimpata akiwa na umri wa miaka 13 baadae mumewe alifariki kwa kutumbukia kisima cha nyumbani kwake akiwa anasafisha na hapo maisha yakawa magumu maradufu,said a alieonekana kuhuzunishawa na kifo cha mumewe kwani alikiri kuwa yeye ndio alikua kioo na mwanga wake ktk maisha ya kisasa kwa kumgundisha vitu vingi ambavyo alikua havijui.

Anaamini hali hiyo ya kutosoma ndio iliyompelekea yeye kuishi vibaya has a wakati alipokua ktk harakati za mziki kwani alikua hawawezi hata kujaza mikataba kwakua hajui kusoma wala kuandika,hata hivyo halo hiyo kwasasa ameiondoa kwa kiasi kikubwa kwa kuamua kutafuta mwalimu wake binafsi nakufundishwa kusoma na kuandika akiwa nyumbani.

Mara kadhaa Saida karoli alidiliki kutaka kujiua kwa kujinyonga,kunywa sumu  na vidonge Ila mungu alimuokoa kwa watu kumfuma kabla ya kutekeleza matukiko hayo na kumuokoa,sababu za kufanya mambo hayo kubwa zilikua ni kupoteza Dora ktk Sana'a na maisha kwa ujumla na asijue nini  cha kufanya has a kwa pigo la  kufiwa na mumewe.

Said a ambaye alikiri licha ya kusafiri na kufanya matamasha makubwa sehemu nyingi wakati akiwika ktk Sana'a yeye hakufanikiwa kuwa na nyumba au Mali yeyote ya maana iliyotokana na kazi yake  hiyo na hivyo kupelekea yeye kujiona hana sababu ya kuishi,pia saida alizungumza kulishwa sumu ambayo ilimfanya kubadilika hali ya mwili wake na kuambiwa na daktari hatoweza kuzaa tena japo haikuwa hivyo.

Saida pia alizungumzia swala la mwanamuziki Diamond kuimba wimbo wake wa Salome upya na Darasa kuingiza kipande cha wimbo huo Nitakuchambua kama Katanga kuwa yeye hana tatizo nao japo hawakuomba ruhusa Ila anaamini wao ndio wamemuahamasisha kurudi tena ktk tasnia ya mziki.

Mwanamziki huyu alioneka kukiri kuishi maisha magumu sana kipindi cha kati na kufikia kiasi cha kukata tamaa na kujaribu kujitoa uha Mara kadhaa na kuzushiwa na kufa Mara kadhaa.

Said a karoli amekusudia kurudi ktk fani ya mziki kwa kishindo kwani roho ya kukata tamaa imeshaondoka,sauti ya msanii huyu bado iko vilevile kama ya kasuku na ilishangaza sana kwa kipaji cha ajabu alichokua nacho dada huyu kwa kuweza kukariri na kuimba nyimba ndefu zenye maneno yankiswahili na kihaya licha ya kutojua kusoma wala kuandika kipinda cha mwanzoni.




Share :

Facebook Twitter Google+
1 Comment "SAIDA KAROLI AZUNGUZA UKWELI KUHUSU MAISHA YAKE"

Nakupenda sana saida karoli..naomba namba yake ya simu niweze kuwasiliana nae ..my contact 0620217351

Back To Top