Ile ahadi ya Rais John Joseph Magufuli ya kuhamishia serikali yake Dodoma ambao ndio mji Mkuu wa Tanzania inaonekana kutekelezeka so kwa maneno peke yake Bali kwa vitendo pia!Ni baada ya kuhamisha Ofisi za waziri mkuu na wizara zaidi ya 18 kutoka Dar es salaam kwenda ktk mji huo ambao ulishatangazwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere toka miaka ya 1970 na kusuasua kutokana na sababu za hapa na pale.
Lakini kwa awamu hii ya tano imekuwa picha tofauti na tuliozoe kuiona na kuisikia kwa kuanza kuifanyia kazi ahadi hii iliyo na zaidi ya miaka 40 toka kuamkwa kwake.
Leo Rais Magufuli ametembelea eneo ambalo ikulu ya Dodoma itajengwa ili kujionea mataarisho ya awali ambapo aliona kiwanda cha kufyatua tofauli vijana wakiendelea na kazi ya kutaarisha tofali hizi zitakazotumika kujenga majengo ya ikulu na ofisi mbalimbali.
Rais amekagua matofali hayo na kusaidia kurusha simenti ndani ya mashine ya kutengeneza tofauli,Baada ya hapo Mh.Magufuli aliongea na wananchi waliokuwepo eneo hilo kwa kuwambia kuwa serikali lazima ihamie Dodoma na itejenga miundombinu yote ya msingi kama barabara,reli,kuleta maji na umeme kwenye maeneo ya jirani na ikulu.
Aliwa aliwasisitiza wananchi wa Dodoma kuendelea kujitaarisha na ujio huo mzito kwa kujenga nyumba nzuri kutokana na pesa za fidia watakazolipwa watu chukuliwa maeneo yao kutokana na upanuzi wa mji huo.
Mji wa Dodoma kwasasa unaendelea kujengwa kwa kasi kubwa kutokana na ujio wa wizara mbalimbali kuhitajika kwa majengo ya ofisi na nyumba za wafanyakazi.



0 Comments "SAFARI YA MAKAO MAKUU DODOMA YAIVA"