ARCTIC LAMPREY:SAMAKI ANAYEISHI KWA KUNYONYA DAMU PEKEE

Kumekuwa na viumbe vingi vya ajabu na vya kuweza kukushangaza kwa maumbile yao,vyakula na hata maisha yao ya ajabu,kuchekesha na hata kuwezesha watu kuogopa kabisa.

wataalam wa mambo ya dunia wanasema zaidi ya viumbe 12000 vya ulimwenguni vinaishi ktk maji na 6000 pekee ktk ardhi au nchi kavu,ktk maji kuna viumbe vidogo kabisa ambayo hata kwa mamcho huwezi kuviona kama virusi na bakteria na kuna vile vikubwa kabisa kama papa na nyangumi ambao.

Sehemu zaidi ya 71% ya dunia ni maji matupu na 29% tu pekee ndio ardhi tunayoishi,kulima na kufanya kazi zote,hivyo utagundua kuwa sehemu yenye maji ni kubwa zaidi kuliko nchi kavu.

Imezoeleka kuwa katika maji baridi kama ya mto,ziwa,mabwawa na yale ya maji chumvi kama ya bahari kuishi samaki wa aina mbalimbali laikini hii si kweli kuwa kila kiumbe kinachoishi ktk maji basi lazima kiwe samaki.

Kuna viumbe vilivyojaaliwa kuishi shemu zote mbili yaani nchi kavu na ktk maji na wale wanaoweza kuishi ktk maji baridi na hata maji chumvi kama samaki ajulikanae kama salamanda.

Samaki Arcic lamprey ni samaki wa aina yake kidogo kwa taibia na maoumbile yake yenye kutisha na kushangaza samaki huyu mwenye asili ya kupatikana jimbo la Alaska huko marekani kwenye mito na bahari zenye maji barid yenye kufikia hatua ya kuganda kaisa wakati fulani.

Samaki huyu ni mrefu wa kufikia urefu wa mita moja na ana mwili laini na wenye kuweza kukunjika na kwa kwetu afrika samaki huyu ufanana na samaki aitwae kambale,samaki huyu pia hufanana na ruba ambae mara nyingi huwa kama mnyoo na upendelea kuishi ktk matope na wakati mwingine uingia ktk maji na kuanza kusaka chakula.

Chakula kikuu cha samaki huyu ni damu inayopatikana kwa viumbe wengine wa majini kama samaki na hata wakipata nafasi ya kukutana na binadamu basi pia uweza kunyonya damu na kuganda ktk mwili wa kiumbe huyo kwa mda mrefu akiendelea kufyonza dmu hiyo,wakati fulani anaweza kusababisha kifo kwa kiumbe anayemnyonya damu.

Samaki hawa pia wako ktk mto illinoi,chena na wameshasababisha matatizo makubwa kwa samaki na viumbe wengine waishio ktk maji hayom kwa wanawaua sana na kufanya kuonekana hatari endapo kama watafanikiwa kufika ktk maziwa makuu matano,kwasasa wamewekewa uzio wa umeme ktk mito hiyo ili wasiweze kupita kuelekea ktk maziwa hayo.

Lamprey ni samaki anasadikika kuwepo zaidi ya miaka milioni 360 iliyopita na mpaka sasa yupo na kuendelea kufanya mangamizi makubwa,wataalam wa mambo ya viumbe kuanza kuwasaka na kuwapoteza viumbe hawa hatari.

Samaki jike wa aina hii ana uwezo wa kutaga mayai(100000-170000) na mda mchache tu baada ya kutaga mayai hayo mengi kabisauwa anaweza kufa.






Baadhi ya picha amabazo zinazonyesha samaki huyo anavyoweza kuleta vidonda na hata vifo kwa samaki wenziwe baada ya kuwanyonya damu na kuingia ndani ya miili yao.

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "ARCTIC LAMPREY:SAMAKI ANAYEISHI KWA KUNYONYA DAMU PEKEE"

Back To Top