
Madereva na utingo hao wapatao zaidi ya 23000 wanakuwa hatarini baada ya malori 11500 kushindwa kuingia barabarani kwa kukosa bidhaa za kusafirisha kwenda maeneo mbalimbali,kuna malori zaidi ya 21000 yaliyo sajiliwa kufanya kazi hiyo.
Licha ya kuboreshwa kwa utendaji kazi na miundombinu ya bandari hiyo ya Dar es salaam hasa ktk kipindi hiki cha awamu ya tano kwa kupunguza vipingamizi vya jinsi ys kutoa mizigo ndani ya bdandari hiyo vilivyokuwa vimeambatana na ufisadi,rushwa na uzembe ktk utendaji kazi bado hali inaonekana kuwa tete.
Hadi kufikia mwaka 2015 mwishoni malori mengi yalikuwa barabarani kiasi cha kuleta msongamano wa magari ndani na nje ya jiji ya dar es salaam na kupewa ratiba ya kuingia ndani ya jiji hilo,serikali ilizungumza kuwa ujenzi na uboreshaji wa reli unahitajika ili kupunguza msongamano wa magari,uharibifu wa barabara,mlundikano wa mizigo bandarini.
Kulikuwa na ukwepaji mkubwa wa kodi za serikali kwa mizigo ya wafanyabiashara wengi na kufanya kuingiza mizigo kwa kiasi kikubwa kwa kupitia njia za panya.
0 Comments "MADEREVA NA UTINGO WA MALORI HATARINI KUKOSA AJIRA"