Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu kubwa ya bara la marekani ya kusini au latin amerika zimeendelea kuleta maafa makubwa kwa nchi zinazopatikana ktk ukanda huo wa nchi zenye misitu minene ya mvua(Rain forest),hivi karibuni mvua kubwa zilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya mji wa santiago huko Chile.Peru nayo imekumbwa na mvua kubwa juzi na jana zilizoleta uharibifu na vifo vya watu 62 na wanyama na kubomoa nyumba nyingi na kuwaacha watu wapatao zaidi ya 12000 elfu bila makazi na kuahangaika hovyo.
Miongoni mwa mambo makubwa na ya kushangaza ktk mafuriko hayo ni pale mwanamke ajulikanae kwa jina la avengilina Chommoro mwenye umri wa miaka 32 alivyoweza kuepuka kifo ktk mazingira magumu akiwa ktk maji mazito yaliyochanganyika na matope,miti na uchafu wa kila aina kuweza kuonekana akitembea juu ya magogo hayo yanayosukumwa kwa kasi na kufanikiwa kutoka nje akiwa amefunikwa kwa matope mwili mzima na kutoka akiwa salama.
Ikumbukwe mataifa ya marekani ya kusini kama brazili,chile,bolivia,venezuela ni miongoni mwa mataifa yanayopata mvua za wastani wa juu sana duniani kutokana na kuwepo kwa misitu na milima mingi
Tazama video hii ya mwanamke aliyenusurika kifo.http://video.news.sky.com/video/h264/vod/374/2017/03/DIG160317PERUMUDSLIDERESCUE1489679041180374.mp4


0 Comments "MVUA KUBWA ZISAFISHA PERU KWA MAFURIKO"