JPM:RUKSA KUOA AU KUOLEWA BILA VYETI VYA KUZALIWA

Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli amefutilia mbali agizo lililotolewa na waziri wa sheria na katiba Mh. Hudson Mwakyembe mda mchache tu baadaya kutangazwa ktk vyombo vya habari kwa kuwaagiza wakuu wa wilaya na viongozi wa dini mapadri na mashekhe wote kutofungisha ndoa yeyote ile kuanzia tarehe 1 mei ila kwa sharti la wanandoa hao kuwa na vyeti halali vya kuzaliwa kwa wanandoa hao.

Agizo hili limeleta sintofahamumkwa watanzania kwa kujiuliza kwa maswali mengi juu ya tamko hili ktk maswala haya ya vyeti vya kuzaliwa kwa muoaji au muolewa ktk ndoa za kidini,kimila au kiserikali kwani ni mambo ya kidini.

Izingatiwe kuwa ni asilimia 20% tu ya watanzania wote wevye kumiliki vyeti hivyo vya kuzaliwa kutokana na wengi ya watu kuzaliwa maeneo ambayo huduma hizo hazipo hadi wilayani ana makao makuu ya mikoa,mizunguko mikubwa ktk upatikanaji wake,kutokuwa na ufahamu juu ya umuhimu wake,utunzaji duni na kusababisha kwa kupotea,kuzaliwa nje ya vituo vya afya na hospitali.

Kwa Usumbufu huu ktk swala hili na kutojipanga kwa watu kwa mda mfupi huu uliowekwa na waziri huyo wa sheria na katiba Rais Magufuli amesema agizo hili linahitaji mda na pia ni vyema kupitia bungeni kama mswada kish baadae liwe sheria rasmi endapo litapitishwa.

Rais Magufuli amestushwa sana na gizo hilo na kusema wakati mwingine hata wakuu wa mikoa au hata yeye waziri mwakyembe inawezekana hawana vyeti vya kuzaliwa,kinachohitajika ni kuhamasisha watu wachukue vyeti vya kuzaliwa.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JPM:RUKSA KUOA AU KUOLEWA BILA VYETI VYA KUZALIWA"

Back To Top