NINI MAANA YA TAIFA KUWA TAJIRI? JE WAJUA VIGEZO KWA TAIFA KUITWA TAJIRI?

Katika dhana nzima ya utajiri wa mtu au taifa ni hali ya mtu au nchi fulani kumiliki rasilimali kama madini,mbuga za wanyama,ardhi,majengo na vyanzo vyote vya mapato kwa ajili ya kunufaisha mtu au taifa husika kwa ajili ya kutatua shida na changamoto zao mbalimbali zinazowasibu ktk maisha yao ya kila siku.

Kwa mtu mmoja mmoja unapozunguzia utajiri utakuwa na maana ni hali ya mtu huyo kuweza kumiliki mali ikiwemo majengo,pesa,ardhi na vitu vya thamani ambavyo ktk hali ya kawaida uhitajika na mwanadamu ili kukidhi haja zake za kila siku za maisha yake.

Unaposema taifa fulani tajiri basi utakuwa na maana kuwa watu wanaoishi ndani ya nchi husika wao wana uchumi wa juu kiasi mtu mmoja mmoja au nchi inajitosheleza yenyewe kwa 95% ya shida na changamoto zake ina uwezo wa kuzikabili yenyewe bila kuhitaji msaada kutoka nje.

Nchi nyingi zimejaaliwa kuwa na wingi wa rasilimali za thamani kubwa kama madini,gesi,misitu,bahari,mbuga,ardhi yenye rutuba,maziwa na mito ila kutokana na kushindwa kutumia vyema kwa rasilimali hizo zimejikuta zikionekana ni nchi dhaifu na watu wake wanaishi ktk umasikini uliopindukia mipaka mfano wa nchi hizo ni kama Tanzania,Congo DRC,Somalia,Angola,Nigeria na nchi nyingine kutoka bara ulaya,amerika ya kusini na asia.

Miongoni mwa vyanzo vya kushindwa kutumia rasilimali hizo vyema kwa ajili ya kunufaisha watu wao ni Uongozi mbaya,rushwa,mipingo duni ya maendeleo,kutotilia mkazo ktk miapango yao,elimu duni itolewayo ktk vituo vya elimu,vita za wenyewe,ubinafsi,ukabila,ukanda,kutojitoa kwa ajili ya Taifa husika,kuwepo kwa viongozi vibaraka kwa mataifa mengine makubwa ndani ya nchi.

Tunapoitazama china,india ni miongoni mwa matifa yaliokuwa duni sana ktk uchumi na maendeleo ya watu na hata nchi zao kwa ujumla ukianzia miundombinu kama barabara,maji,umeme,elimu duni lakini ktk karne ya 19 tumeshuhudia mataifa haya yakianza kunyanyuka kwa kasi kubwa sana kiasa cha kuanza kushindana kiuchumi na mataifa mengine ya ulaya. Kwani mapaka sasa china na india wameweza kutengeneza vifaa na mitambo mabalimbali ya kisasa na hata magari na kuuza kwa wengine kampuni kama HUAWEI,TECHNO,TATA,BAJAJ,JIANFANG,FATON,ZONGTONG,YUTONG zikitokea huko lakini pia wameshakuwa wako mbali sana ktk mambo ya utafiti wa anga na mawasiliano na kupeleka vyombo vingi huko.

Kwa mataifa yeyote yalio makini hawafanyi jambo bila kufanya utafiti wa kina ili kupanga litakuwaje,litafanyika wapi,na nani,lini? utafiti ni miongoni mwa mambo ya msingi sana ktk dhana ya maendeleo na yana gharama kubwa sana za fedha na hata ikiwezekana roho za watu,Marekani walipoanza kufanya mapango wa kwenda mwezini walitengeneza vyombo vingi vilivyofahamika kama Appollo 1-13 mwaka 1969 wakafanikiwa kufika mwezini lakini kabla ya hapo walishapoteza vyombo na watu wengi kutokana na ajali za kulipuka kwa roketi zao.

Utajiri wa nchi unaweza kupimika kwa mambo yafuatayo:. ikiwemo Barabara nyingi na bora,uwezo wa wananchi kuishi vyema,huduma bora za afya,mazingira bora ya kazi,kuendelea ktk mawasiliano na usafiri na miundombinu yake kwa ujumla,wananchi wake kuishi ktk maisha bora kwa kuwa na nafuu ya maisha kutokana na upatikanaji wa mahitaji yao kwa wingi,karibu na kwa bei nafuu,kutoa huduma za elimu kwa kiwango kianachohitajika,kuweza kuatatua matatizo yao ya ndani bila kutegemea misaada kutoka pengine,kutumi rasilimali zao kwa ajili ya maslahi yao.

Maendeleo ya mtu,watu au taifa lolote yanaweza kufanikiwa kwa haraka,ufanisi na ubora wa hali ya juu kutokana na utawala husika wa watu hao kwani ndio dira yao ya kila kitu.

Afrika tumekuwa watu wa kuomba,kupewa na kunyenyekea mataifan mengine kula uchao bila ya kuwa na sababu ya msingi,tukisoma history tunaambiwa kuwa mpaka kufikia karne ya 15 waafrika na ulaya wote tulikuwa ktk nafasi moja ya maendeleo. sasa wapi wenzetu walipotupitia? wapi tulilala mpaka tulipoamka tukawa hatuwaoni tena?

 Najiuliza mbona simu kompyuta na magari tunayatumia kutoka kwao ila sisi mbona hata kuiga kutengeneza ya kwetu tunashindwa? Nini shida chuma cha kutengenezea,mekyuli,plastiki,umeme au kipi ambacho kinakosekana afrika kinachofanya kushindwa japo kuiga?

 Je ni kweli tumeridhika waafrika na maisha ya kukebehiwa,kunyanyaswa,na kutumia vya wenzetu tu? Wangapi waafrika wanajaribu kubuni vitu mbalimbali mbona naishia kuwaona wanatangazwa ktk runinga tu alafu siwasikii milele daima? wanapotelea wapi watu wale wanaojaribu kuonyesha njia za maendeleo kwa vitendo?

Nimegundua Tatizo kubwa ambalo linatumbua liko vichwani kwetu! kwani Wataalam yale azungumzayo au kutenda mtu ndio uhalisia wa mawazo yake yaliyo kichwani mwake. Hivyo waafrika kamwe hatutabadilika kivitendo na maendeleo mpaka pale tutakapobadilika vichwani kwetu!

Miongoni mwa mambo ambayo watu weupe hawahitaji mtu kuwachezea kwa hayo ni umoja na amani ya nchi zao, Tumeona nchi nyingi za ulaya na marekani zikichukua hatua ngumu na nzito kwa wageni kwa ajili ya kulinda usalama wao. kwanini? Amani ndio mzizi na shina la watu kuendelea mbele.

Mfano mdogo familia au wanandoa ambao wao hawana amani kutokana na sababu mbalimbali basi daima hawatokuwa na maendeleo na kama watakuwa nayo basi pindi migogoro inapoanza tu ndio inakuwa mwanzio wa kuporomka kwa maendeleo hayo na kuwa duni kabisa kuanzia wao na watoto zao.

Hii itakuwa tofauti kabisaa na familia iliyotulia kimaisha ni rahisi sana kuendelea.





Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "NINI MAANA YA TAIFA KUWA TAJIRI? JE WAJUA VIGEZO KWA TAIFA KUITWA TAJIRI?"

Back To Top