JPM ATEMA CHECHE

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania leo akiwa ktk shughuli ya kuapisha mawaziri wawili wapya aliowateua jana asubuhi baada ya kutengua uteuzi wa waziri wa michezo na habari Mh.Nape Nnauye na ule wa Waziri wa sheria na katiba Mh. Harrison Mwakyembe.

Nafasi hizo zikajazwa upya na Mh.Palamagamba Kabudi kuwekwa wizara ya michezo na habari na Mh.Harrison Mwakyembe kurudishwa upya ktk wizara Habari,michezo,sanaa na utamaduni na Mh. Nape kuachwa.

Leo 24/3/2017 Rais Magufuli akiwa ikulu na viongozi na mabolozi wapya wateule kutoka mauritius,belarus na kwengineko alikuwa na shughuli ya kuapisha Waziri wa Michezo na sanaa  Mh.Palamagamba Kabudi na Mh.Harrison Mwakyembe ili kushika rasmi nyadhifa hizo.

Aidha Rais Magufuli alivishutumu vyombo vya habari kwa kupenda kuandika zaidi habari mbaya na za matatizo pekee kurasa za mbele kuliko mambo mazuri na ya msingi ktk jamii.

Rais ametoa mfano swala la jana la askari kutoa bastola kwa Mh. Nape Nnauye hiyo habari imeandikwa na vyombo vyote vya habari tena kurasa za mbele,Rais amesisitiza kuwa uhuru uliopitiliza mipaka kwa vyombo vya habari uliopitiliza mipaka unaweza kuleta matatizo kwa jamii kwa kuleta migogoro kwa serikali na jamii nzima,Kwani vyombo vya habari vimekataa kurusha au kuandika habari za muheshiwa fulani lakini napofanya mabaya ndio yanrushwa peke yake.


Pia amemsisitiza Mh.Harrison Mwakyembe kuwa akapige kazi zaidi kwani yeye amesomea sheria na habari hivyo anao ujuzi na uwezo mzuri zaidi kwa sekta hiyo,Rais amesisitiza watu kuwa wamoja na kuachana na mambo yasiyoleta tija kwa maendeleo ya taifa na watu wake




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JPM ATEMA CHECHE"

Back To Top