NEY WA MITEGO MIKONONI MWA POLISI MOROGORO

Msanii wa kizazi mziki wa kizazi kipya maarufu kama bongo fleva mwenye maskani yake manzese jijini Dar es salaam ametiwa nguvuni na polisi akiwa mkoani morogoro ktk shughuli zake za kawaida za kimuziki na hadi sasa hajaachiwa
Msanii huyu alikuwa mkoani humo toka jana na alifanya onyesho la nyimbo zake na kuimba nyimbo zake nyingi ikiwemo na ile mpya ya (WAPO) iliozua gumzo ktk mitandao ya kijamii kwa vijana wengi,kwa kuhisiwa kama inataja viongozi fulani ktk mamlaka.

Watu wengi wanahusisha kukamatwa kwake na juu ya nyimbo hiyo hsa kwa maudhui iliyonayo,msanii huyu anafahamika kwa kwa kuimba nyimbo zenye maneno ya kibabe na yaliyo wazi kwani baadhi ya nyimbo zake zimekuwa zikizuiwa kutoka ktk vyombo vya habari na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA).




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "NEY WA MITEGO MIKONONI MWA POLISI MOROGORO"

Back To Top