
Mhusiano haya si mageni ktk dunia hii kwani yalikuwepo toka kuumbwa kwa wanadamu,hat viumbe wengine wana mahusiano haya ila yana tofauti kubwa kati ya kwetu wanadamu na viumbe vyengine visivyo sisi.
Tofauti kubwa hiyo inatokana na kuwa viumbe wengine wote wao wanakuwa na mahusiano haya kwa ajili ya kendeleza vizazi pekee na ndio maana mahusiano yao ya kimapenzi wanayatenda kwa mda maalum,kwa mafano tuanalie wanyama na ndege weni wao hufanyamambo haya ya kimapenzi kwa nyakati maalum tu ili kupata ujauzito au kuataga mayai na baada ya tendo hilo hakuna mwendelezo mwingine wa tendo hilo mapaka pale watakapopata viumbe wenzao. Tendo hilo halitorudiwa tena hadi pale mda kama huo utakapofika tena.

Hii ni tofauti kabisa na wanadamu kwani wao wanakuwa na ndoa au mahusiano kwa ajili ya Starehe,kuongeza kizazi(watoto),kusaidiana ktk maisha na kutimiza kusudio la mungu. Na matendo haya uendelea kufanyika hata baada ya ya kupata ujauzito na pia kila mmoja wao uwa na mtu wake maalum wa kutenda nayo hayo mambo na haya yako tofauti na kwa wanyama ambao wao hawana utaratibu wa kuwa na mmoja maalumu wala cha huyu mama,dada au shangazi wao hata mama anaweza kujaniiana nae.
Wanadamu tumeumbwa na kuwekwa duniani kwa utaratibu maalum wa kuishi kwa mujibu wa imani za kidini na elimu za kidunia.
Ndoa kwa maelezo ya kawaida ni mkataba maalum unaofungwa baina ya mwanamke na mwanamme kwa ajili ya kuishi,kushirikiana ktk maisha pamoja ili kuendeleza kizazi na kutimizamkusudio la mungu.

Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia ili kufanya mahusiano yetu ya kindoa kudumu na hatimae kutimiza lengo ambalo lilikusudiwa na mumgu na wanandoa wenyewe.
1.Ni vyema kuoa au kuolewa na mtu ambaye manashabiana au kufanana ktk mitazamo ya kidini(kiimani),kimila,desturi.
Kwani hii ni miongonuinmwa nguzo muhimu ktk maisha ya kimahusiano.wengi hujikuta ktk matatizo makubwa mbele ya maisha ya ndoa,kwani mara ya kwanza alivutiwa na mtu na hivyo hakufuata miiko hiyo ya msingi. kumbuka ndoa sio mahala pa maigizo au pa kupita tu.
2.Kujua kusudio la ndoa na mahusiano kwa kina kwa wanandoa wote(kwanini uko au unaingia ktk ndoa) hii ni elimu muhimu sana.

3.Ingia ndani ya ndoa au mahusiano ukisukumwa na kuishi maisha na sio kuvutiwa zaidi na mambo mengine kama maumbile,kipata aha uchumi wa mtu husika kwani kama hayo unayoyataka siku moja yanaweza kupotea.
4.Zingatia malezi na ndugu na jamaa ambako unakwenda kuoa au kuolewa kwani mara nyingi kizazi cha mtu unaekwenda kuishi nae ndio kitakuwa ni sehemu ya maisha yenu.
5.Kuvumiliana ktk misukosuko ya kimaisha kama kukumbwa na maradhi makubwa,upotevu wa viungo,kushuka kwa kipato au uchumi,na kusaidiana ktk kupeana mawazo chanya ya kutafuta maisha.
5.Kuwa na lengo,usudio,mtazamo mmoja na kuacha ubinafsi ktk kumiliki na kutafuta mali mali na kuona kila mtu anakuwa na vya kwake au kila mtu anafanya mambo kwa faida binafsi na kusahau kabsa kuwa nyie lenu ni moja.
6.Kuacha kuadanysa mwanzoau ndani ya mahusiano kwani kila mtu anavyogundua kuwa
ulimdanganya uatakuwa uanapunguzan asuilimiam fulani ya uaminifu.
7.Uwazi ktk matumizi ya simu na vitu vyengine vya utandawazi,ambavyo kwasasa vinahusika ktk uvunjifu wa ndoa kwa kiasi kikunbwa sana.
8.Kuwa na subira na uvumilivu pindi inapotokea kukoseana ni muhimu sana kusamehe amkosa hayo ikiwa ni ya kawaida.
9.Kutafuta suluhun na ushauri kwa watu makini walio ktk ndoa mda mrefu pindi inapoteokea kukosana ndani ya ndoa kabla yakuchukua hatua ngumu na za haraka.
10.Wandoa hawatakiwi kuishi kwa kuiga kila wanaloliona kwa watu wengine,ni muhimu san kuwa makini na kuishi kwa jinsi mlivyo nyinyi,kwani maisha ya ulimwenguni yako tofauti sana,kuiga ua kupokea kila ushauri ktk mahusiano yako na kataka kuyafuata hayo ni hatari wakti mwingine.
11.Ni muhimu kusikilizana na kuelewana ktk mambo manayotakiwa kushaurina.
12.Kuchunga mipaka na sheria za ndoa(heshimautii,adabu,subira).

14.Kuwa na usiri mkubwa ktk mipango na badadhi ya matatizo ya ndoa zenu na ikiwa yatazidi basi ni muhimu kwenda kupata ushauri kwa watu maalum kama wazazi na viongozi wenu wa kiimani au watu walio kwenye ndoa kwa mda mrefu na wenye hekima ktk jamii.
15.Yako mambo mengine yanayoweza kuchangia uvunjikaji wa ndoa kama(uongo,marafiki usiofanana nao kimawazo,mtumizi ya vilevi kama pombe n.k)
16.Ni muhimu kwa mke na mume kufanya ziara au matembezi kwa wanandoa wenzao kwani inawea kusaidia kubadili baadhi ya mambo kwa kuona wanavyoishi wezenu

Ikiwa kweli inafika mahali licha ya kuomba ushauri,mawazo bado kutakuwa na mvurugano au mwendelezo wa tabia chafu ndani ya mahusinao yenu basi i muhimu nani bara zaidi kutengana au kuacha kwa amani ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kuja kutokea mbela ktk maisha yenu kama mauaji,kuambukizana magonjwa,kuaharibu mustakabali wa maisha ya watoto.

Wataalam wa mambo ya ndoa na mahusiano wanasema ndoa ya kwanza inakuwa nasilimia 40% ya kuvunjika wakati ya pili ina 60% na ile ya tatu uwa na 80% ktk kuharibika na kuvuniijka.
0 Comments "JE WAJUA SABABU ZA NDOA AU MAHUSIANO KUGEUKA TAMU AU SHUBIRI?"