WIMBO MPYA WA NEY WA MITEGO SASA HURU KUPIGWA KTK VYOMBO VYA HABARI

Msanii Ney wa mitego aliyekamatwa mkoani morogoro usiku wa jumamosi kuamkia jumapili wiki iliyopita,ameachiwa huru leo baada ya kushikiliwa na polisi kwa siku mbili mfululizo kwa kosa la kutunga na kuimba nyimbo yake mpya aliyoipa jina la (WAPO).

Nyimbo hii yenye maneno mengi yalionekana wazi kuguza baadhi ya viongozi wa juu na matendo mbalimbali yanayoendelea nchini,Ndani ya nyimbo hiyo alizungumzia mambo y matumizi ya madawa ya kulevya,vyeti fekina aina mbalimbali wa ukiukwaji wa sheria unaofanywa na wananchi na hata viongozi wa juu wa serikali kwa kuonekana kukiuka miiko na maadili yao ya kazi.

Ney wa mitego alisafirishwa hadi alifikishwa kizimbani na kuhojiwa maswali kadhaa juu ya maana na kusudio la wimbo wake hu mpya uliojaa maneno ya mtaani yalijificha kimaana kama malinda,kichaa kapewa rungu n.k.

Waziri mpya wa wa wizara ya Habari,utamaduni ,sanaa na michezo Mh.Harrison Mwakyembe aliyeteuliwa hivi karibuni kufuatia utenguzi wa aliyekuwepo kabla yake Bw. Moses Naper Nnauye amesema kuwa kwa mijibu wa Kauli ya Rais John Pombe Magufuli ameamuru wimbo huo kupigwa na vyombo vya habari vyote kwani unaonekana kuwa na maudhui na jumbe nzuri kwa jamii na kumuomba labda kufanya marekebisho ya hapa na pale ili kuifanya kuwa nzuri zaidi.

Msanii huyo ameachiwa huru na kuruhusiwa kuutumia wimbo wake huo popote bila shaka yeyote ile


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "WIMBO MPYA WA NEY WA MITEGO SASA HURU KUPIGWA KTK VYOMBO VYA HABARI"

Back To Top