Jana machi 24 Rais Magufuli amewaapisha mawaziri aliwateua juzi ktk barua rasmi ya ikulu iliysema kuwa Rais Magufuli amemteua Dk.Harrison Mwakyembe kuwa waziri wa Habari sanaa na michezo nafasi ilyokuwa ikishikwa na Moses Nape Nnauye kabla ya kutenguliwa kwake siku hiyo na pia alimteua Palamagamba kabudi kuwa waziri wa Sheria na katiba nafasi iliyokuwa ikishikwa na Dk.Harrison Mwakyembe kablaya kuenguliwa kwake.Rais Magufuli alimsisitiza Mwakyembe kwenda kufanya kazi na kushughuikia matatizo yote yanayolalamikiwa kwa nguvu zote na anamuamini yeye kwakuwa amesomea mambo ya habari na sheria hivyo anatumaini atafanya vyema ktk wizara hiyo.
Rais alisema alisikia kuwa aliona ktk mitandao ya kijamii kuwa Yeye hatokwenda kuapishwa baada ya uteuzi ule wa juzi kwakuwa atagoma kupokea nafasi hiyo lakini kwa bahati nzuri hakuiwa hivyo kama mitandao ilivyosema kabla.
Mwakyembe ameahidi kwenda kuifanyia kazi ripoti hiyo iliyoachwa na waziri wa zamani Moses Nape Nnauye juu ya uvamizi wa kituo cha matangazo ya runinga cha clouds mikocheni na kundi la askari wakiongozana na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

0 Comments "MWAKYEMBE MTEGONI: KUANZA NA RIPOTI YA NAPE"